loader
Dstv Habarileo  Mobile
Urusi kufungua viwanda vya dawa Afrika

Urusi kufungua viwanda vya dawa Afrika

URUSI imesema itasaidia nchi za Afrika kufungua viwanda vya kutengeneza dawa za tiba za binadamu na kwa kuanza viwanda hivyo vitaanzishwa Ivory Coast na nchi jirani.

Akizungumzia hatua hiyo, Waziri wa Viwanda wa Urusi, Denis Manturov (pichani) alisema hiyo ni hatua mojawapo ya ushirikiano wake na nchi za Afrika. Alisema kuwa wanategemea viwanda hivyo, vitakuwa zikitengeneza dawa hizo kwenye nchi husika na kuzisajili.

“Tunapozungumza kuhusu viwanda vya kutengeneza dawa za tiba za binadamu katika nchi za Afrika, tunakusudia kuzalisha pia vifungashio vya dawa kama vile chupa na mifuko tuko mbioni kusajili na kuanzisha kiwanda cha dawa nchini Ivory Coast’’, alisema Manturov.

Alisema idadi ya watu nchini Ivory Coast ni milioni 25. Alisema kwamba asilimia mbili ya watu hao hawana ajira huku mfumuko wa bei ukiwa asilimia 0.5 huku uchumi wa nchi hiyo ukikua kwa asilimia 7.5 kwa mwaka.

“Hii ni nchi yenye matumaini, ina uchumi unaokua vizuri, tunataka kushirikiana nao,” alisema Manturov.

Waziri huyo alitoa mwito kwa Kituo cha Utafiti wa Sayansi ya Kinga cha Chumakov kusambaza dawa moja kwa moja kwenye nchi za Afrika, kwa kuwa Urusi imeamua kuimarisha zaidi uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na nchi hizo baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kimataifa wa Urusi na Afrika, uliofanyika mwezi huu mjini hapa.

“Tunafanyia kazi masuala ya kinga na dawa za saratani, tunaanza na kiasi kidogo kwa sasa lakini tumekusudia kuwa wasambazaji wakubwa wa uhakika wa dawa hizo, ugumu unatoka tu pale mwanzoni wakati wa kusajili dawa, ila tunafanyia kazi ugumu au changamoto hiyo,” alisema Manturov.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/eab525ff4129c4a3d7283c4fa9d877f2.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: SOCHI, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi