loader
Makonda- Idris Sultan jisalimishe Polisi

Makonda- Idris Sultan jisalimishe Polisi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemtaka mchekeshaji Idris Sultan aende kituo cha polisi atakuta ujumbe wake.

Katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kijana huyo ameandika maneno 'Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani'.

Katika post hiyo ameweka picha mbili mojawapo ikimuonesha yeye akiwa amekaa kwenye kiti cha Rais Ikulu na nyuma ya kiti hicho kuna bendera ya Rais.

Picha nyingine inaonesha mtu mwenye sura ya Rais akiwa amevaa saspenda.

Jana ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Rais John Magufuli.

"Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako. @idrissultan" ameandika Makonda kwenye ukurasa wake wa kwenye mtandao wa kijamii wa instagram.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c0a592290fd004fa3af7d73ba225fde8.jpeg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi