loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC ataka Tanesco watekeleze ahadi

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limekutana na wateja wake wakubwa na wenye viwanda Kanda ya Kati na kutakiwa kutetekeleza ahadi ya serikali kwa Watanzania ya kusambaza huduma ya umeme iliyo bora nchini kote.

Mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma jana, ulihusisha wawekezaji wenye viwanda katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge.

Dk Mahenge amesema serikali iliahidi kuwapatia Watanzania huduma ya umeme iliyo bora na yenye uhakika ili kuwakwamua kiuchumi hususan walioko maeneo ya vijijini na kuitaka Tanesco kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwekeza katika miradi mikubwa ya uboreshaji wa miundombinu ya umeme.

Aliitaja miradi midogo na mikubwa inayoendelea kutekelezwa mkoani Dodoma kuwa ni uboreshaji wa kituo kikubwa cha gridi ya taifa cha Zuzu kinachoongezewa uwezo kutoka kupokea megawati 48 hadi megawati 400 ambao unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Dk Mahenge aliwataka wawekezaji kutumia fursa hiyo ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kuwekeza zaidi katika viwanda mbalimbali hasa ikizingatiwa kuwa Dodoma ndio makao makuu ya serikali. “Jiji la Dodoma lina fursa nyingi hivyo ni wakati sahihi wa kuwekeza katika kulijenga jiji,” alisema.

Amewakaribisha wadau wote waliohudhuria kikao kazi hicho kupita katika ofisi ya mkurugenzi wa jiji la Dodoma na kupata maelezo ya uwekezaji kwani hali ya umeme mkoani humo ni nzuri.

SERIKALI imetumia Sh Bilioni 15 kwa ajili mikopo ya pembejeo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi