loader
Dstv Habarileo  Mobile
Moto kwenye treni waua watu 65

Moto kwenye treni waua watu 65

WATU zaidi ya 65 wamekufa na wengine takribani 43 wamejehuriwa baada kutokea mlipuko wa moto kwenye treni leo nchini Pakistan.

Inadaiwa kuwa mlipuko huo ulioteketeza mabehewa matatu umetokea jirani na mji wa Rahim Yar Khan wakati abiria wakipika kifungua kinywa kwenye majiko ya mafuta wakati treni ikiendelea na safari.

Treni hiyo ilikuwa safarini kutoka mjini wa kusini ya Karachi wa Rawalpindi, na kuna taarifa kwamba, abiria wengi walikuwa wakienda kuhudhuria mkutano wa kidini ulioandaliwa na taasisi ya Kiislamu ya dhehebu la Sunni iitwayo Tablighi Jamaat.

Inadaiwa ajali hiyo imesababishwa na kulipuka kwa majiko mawili ya mafuta, na kwamba, abiria kuwa na mafuta ya taa wakati treni ikiwa kwenye mwendo kuliongeza kasi ya kusambaa moto.

Kwa mujibu wa Waziri wa Reli wa Pakistan Sheikh Rashid Ahmed abiria wengi wamekufa kwa kujirusha kutoka kwenye treni.

Picha za zimesambaa kwenye mitandao zikionesha mabehewa ya treni hiyo yakiungua na moshi ukitoka madirishani.

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu ajali hiyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6741d528c3efb1a94ab019fb52c628c5.jpg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi