loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima kurudishiwa mil 300/- za ufuta

VIONGOZI 200 wa vyama 31 vya msingi mkoani Lindi wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa tuhuma za kuhusika kudhulumu sh bilioni 1.23 za wakulima wa ufuta.

Taarifa za awali za Wizara ya Kilimo zimeonesha kwamba fedha zilizodhulumiwa zilikuwa milioni 400/-.

Katika operesheni maalumu ya kufuatilia malipo ya wakulima wa ufuta Takukuru imeokoa zaidi ya sh milioni 300/-, na kwa kushirikiana na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika wamerejesha milioni 152 kwa wakulima wa Lindi.

Katika siku ya kwanza ya kurejesha fedha wilayani Kilwa zaidi ya shilingi milioni 103 zilizoporwa wilayani ya Kilwa zimerejeshwa kwa wakulima hao juzi. Jana ilikuwa zamu ya Liwale.

Taarifa hizo zimo katika hotuba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akirejesha sehemu ya kwanza ya fedha za wakulima katika wilaya ya Kilwa, eneo la Nanjilinji.

Amesema wilaya ya Kilwa na Liwale kwa pamoja wanatarajia kurejeshewa sh milioni 300 na wataendelea na shughuli hizo kwa kadri wanavyozikusanya kutoka kwa wahusika.

Liwale kwa upande wake jana walitarajiwa kulipwa sh milioni 147.

Malipo hayo yametokana na maagizo ya Rais John Magufuli ya kuitaka Takukuru kusaka na kurejesha fedha zote za wakulima walizodhulumiwa na viongozi wao wa Amcos.

Alitoa agizo hilo Ruangwa mkoani Lindi wakati wa ziara hivi karibuni ambako alisikia kilio cha wakulima cha kudhulumiwa ufuta.

Wakati huo Rais Magufuli aliambiwa ni vyama 10 tu vya ushirika vilihusika na dhuluma hiyo na kwamba wakulima walikuwa wamedhulumiwa Sh milioni 400.

Brigedia Jenerali Mbungo amesema, katika uchunguzi Takukuru wamebaini kwamba dhuluma hiyo imetendeka katika vyama 31 vya msingi vya ushirika.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu,Kilwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi