loader
Makonda apokea mil 27/- kulipia bima watoto 500

Makonda apokea mil 27/- kulipia bima watoto 500

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea Sh milioni 27 kutoka kwa Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ajili ya kuwalipia bima watoto 500 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Watoto watakaolipiwa bima hiyo ni wale waliofanyiwa na watakaofanyiwa operesheni ya moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhiwa hundi ya fedha hizo Dar es Salaam jana, Makonda alisema ubalozi huo umekuwa bega kwa bega na serikali katika kusaidia changamoto mbalimbali zinazowapata wananchi.

“Ubalozi huu ni rafiki wa Watanzania, umesaidia kusomesha watoto 100 wa kike, kusaidia kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuturisha misikiti 800, umeleta madaktari 10 kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto Muhimbili na sasa unawalipia bima watoto hawa 500,” alisema Makonda.

Alisema amekuwa na kampeni ya kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo na ndipo kupitia ubalozi huo wa UAE chini ya Balozi wake nchini Tanzania Khalifa Abdulrhaman Almarzooqui walileta madaktari hao 10 kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji watoto wenye matatizo ya moyo.

Alieleza kuwa katika kampeni hiyo jumla ya watoto 60 walifanyiwa upasuaji, lakini ikaonekana kuwa kuna haja ya kuendelea kuwasaidia wazazi wa watoto hao katika kufuatilia maendeleo yao ikiwemo kuwawekea bima.

“Wengi wa watoto hawa na wazazi wao wanaishi katika mazingira magumu, akishafanyiwa upasuaji mzazi atatakiwa kufuatilia afya ya mtoto ikiwemo kwenda kliniki, sasa gharama za yote haya wataiwezaje? Alihoji. Alisema kwa kushirikiana na ubalozi huo wameamua kuanzisha bima hiyo kwa watoto hao 500 ya mwaka mmoja, itakayohusisha watoto hao waliofanyiwa upasuaji na wengine wanaofanyiwa upasuaji hospitalini bila kujali sehemu wanakotoka.

“Mwakani tuna mpango wa kufanyia upasuaji watoto wengine 500 wenye matatizo ya moyo, hawa nao tutawaingiza kwenye mfumo huu wa bima,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9ca98facc71f32fa26ea4def8275c180.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi