loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watanzania wahimizwa biashara kwenye gesi, mafuta

WIZARA ya NISHATI imezitaka kampuni za kizalendo zinazotaka kufanya kazi kwenye kampuni za gesi na mafuta zijisajili kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Ametoa tangazo hilo leo jijini Dodoma wakati anafungua Jukwaa la Tisa la Uziduaji ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) iliyoanza Novemba nne.

“Kajisajili EWURA ili tukutambue ili wanapokuja kuwekeza tunampa maorodha ya makampuni ya ndani, chukueni hapa, chukueni kati ya hawa halafu sisi tunafuatilia” amesema.

“Tunataka kuona nyanya inayoliwa kule Mnazi Bay au Songosongo inatokana na nyanya ya kitanzania. Kama ni mchele ni mchele wa kitanzania unaotolewa na Mtanzania, kama ni maji ni hivyo hivyo, kama ni ulinzi ni hivyo hivyo, kama ni kufagia afagie mwanamama au mwanadada wa kitanzania apatepo kaajira hayo ndiyo mambo tunafuatilia” amesema Waziri Kalemani.

Amewakaribisha wawekezaji kutoka nje lakini waje wakitambua kuwa masuala ya local content (kuthamini vya nchini kwanza/ wa nchini kwanza) hayana mjadala.

“Fursa zipo, sheria ni nzuri, sera ni nzuri, siasa ni nzuri, uchumi unakua wawekezaji wa nje waje wawekeze. Wa ndani watumie fursa hizo kwa sababu zipo kwa ajili yao” amesema Dk Kalemani.

WAKULIMA wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuchangamkia fursa ya  miche ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi