loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara- Tutalinda wachimbaji wakubwa lakini…

WIZARA ya Madini imesema inatoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa sababu wanaongeza mapato kupitia kodi sanjari ya kupanua wigo wa fursa za ajira kwa wananchi.

Naibu Waziri wa wizara hiyo Stanslaus Nyongo amesema leo jijini Dodoma kuwa, Serikali inawategemea wachimbaji wakubwa lakini ni wachache hivyo mmoja akisitisha uzalishaji madhara yake yanakuwa makubwa kwenye pato la nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.

“Tunachukua wachimbaji wadogo wadogo wawe wengi tuwawezeshe ikiwezekana tuwape na mikopo, tuwasaidie kufanya tafiti, tuwasaidie kuwapa vifaa, tuwafundishe, tuwape skills (ujuzi), tuwafundishe uchimbaji salama, tuwafundishe namna ya kuprotect (kulinda) mazingira, wachimbaji hawa wakiwa wengi ile tax base (idadi ya wanaolipa kodi) yao inakuwa ni promising kwa sababu ni wengi na wanakuwa na mchango mkubwa” amesema.

Ameyaema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Azaki (Asasi za Kiraia) iliyoanza Novemba nne.

“Kwa hiyo kwa wachimbaji wakubwa tunawalinda lakini tunatengeneza wachimbaji wadogo wawe wengi zaidi” amesema Nyongo na kubainisha kuwa miongoni mwa mambo ya kuwawezesha wachimbaji wadogo ni kufungua masoko ya madini.

Amesema wachimbaji wadogo wanapewa maeneo kupitia vikundi vidogo vya watu wanaotoka kwenye maeneo husika.

“Wanapewa viwanja vya kuchimba chini ya kamati ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye anakuwa mwenyekiti, na katibu wake ni Ofisa Madini wa Mkoa pamoja na wajumbe wawili kutoka mkoani wanaochaguliwa na RAS (Katibu Tawala wa Mkoa), wao wanasimamia kuangalia wachimbaji wadogo wanawapa maeneo ya kuchimba” amesema Nyongo.

SERIKALI imetumia Sh Bilioni 15 kwa ajili mikopo ya pembejeo ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi