loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanunuzi wakubwa wa dhahabu mbaroni

SERIKALI imekamata wanunuzi tisa wakubwa wa dhahabu waliokuwa wakinunua madini hayo nje ya masoko.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema jijini Dodoma kuwa, tangu kuanzishwa kwa masoko hayo Machi mwaka huu yameongeza mapato hasa katika mauzo ya dhahabu.

Amesema serikali imeua mtandao wa ununuzi wa madini nje ya masoko hayo na sasa wauzaji na wanunuzi wananufaika.

Nyongo amesema hadi sasa kuna masoko zaidi ya 28 ya madini na yana matokeo chanya ya moja kwa moja.

Amesema, soko la madini mkoani Geita limeiwezesha Serikali kukusanya zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwezi kutoka shilingi milioni 440/- hadi shilingi milioni 500/- za awali.

“Ukienda Chunya dhahabu iliyokuwa inakusanywa kwa mwezi ni kilo 20 tu lakini sasa hivi tunavyozungumza kwa mwezi mmoja tunakusanya kilo zaidi ya 150, haya ni mabadiliko makubwa” amesema Nyongo wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Serikali ilianzisha masoko ya dhahabu baada ya kujiuliza mchimbaji anapopata dhahabu anapeleka wapi na mnunuzi anayetaka kununua dhahabu anakwenda kununnua wapi.

“Mnunuzi na muuzaji hawakuwa na maeneo ya kukutana, tukasema ni lazima wanunuzi na wauzaji wa dhahabu tuwatengenezee mahala maalumu wakutane ili kusudi wauziane na wakiuziana Serikali Serikali iweze kuchukua tozo yake pale, ichukue mrabaha, ichukue clearance fee, halmashaur ichukue service levy yake kama kodi ya halmashauri na kwa kweli machimbaji wamefurahia masoko haya”amesema Nyongo.

“WATU wengine wakiona mwanamke mwenye ulemavu ana mimba, wanashangaa na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo na Janeth Mesomapya

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi