loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia aalika nchi SADC kununua viuadudu Pwani

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kukabiliana na malaria, zinunue dawa ya kuua mazalia ya mbu katika Kiwanda cha Viuadudu cha Kibaha mkoani Pwani kwa utaratibu wa manunuzi ya pamoja wa nchi hizo unaoratibiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

Samia amewahakikishia wanachama wa SADC kuwa, MSD imejipanga vizuri kuhakikisha jukumu hilo la uratibu wa manunuzi ya pamoja linatekelezwa kwa ufanisi na kufafanua kuwa, taasisi hiyo sasa inaendelea na hatua ya kusaini mikataba na wazalishaji wa dawa na vifaa tiba.

Aidha, Makamu wa Rais, Samia amesema Tanzania katika kutekeleza Itifaki ya Afya ya SADC ya mwaka 1999, inafanya vizuri katika sekta hiyo ambapo imepunguza kiwango cha malaria kutoka asilimia 14.8 hadi asilimia 7.3 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 na idadi ya maambukizi mapya imepungua kwa asilimia 27 kutoka watu 164 hadi 119 kati ya watu 1,000.

Samia aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa nchi za SADC wanaoshughulika na Sekta ya Afya na Ukimwi, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulioanza Novemba 4 kwa vikao vya makatibu wakuu na wataalamu wa sekta hiyo na kufuatiwa na mkutano huo wa mawaziri unaofanyika jana na leo, umehudhuriwa na mawaziri na wataalamu kutoka nchi 14 kati ya 16 za SADC.

“Ili kutokomeza malaria nchini, Serikali imejenga kiwanda cha kutengeneza dawa ya Viua Dudu chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni sita (6) kwa mwaka. Dawa zinazozalishwa zinatumika kudhibiti wadudu dhurifu wakiwemo viluilui vya mbu wanaosababisha malaria. Nitumie fursa hii kuhamasisha nchi za SADC zinunue dawa ya viuadudu katika kiwanda hiki kupitia utaratibu wa manunuzi ya pamoja unaoratibiwa na MSD,” alisema Samia.

Alifafanua kuwa, kwa mwaka huu (2019) Serikali ilifanikiwa kunyunyiza lita 230,000 katika makazi ya wananchi na kuwataka mawaziri na ujumbe wa SADC utakapotembelea kiwanda hicho leo, wajionee na kujifunza uwezo wake ili wasisite kuchukua hatua ya kununua dawa hiyo. Akieleza namna Serikali ya Tanzania inavyotekeleza lengo la afya kwa wote, Samia alisema imeweka kipaumbele kuimarisha miundombinu na mifumo ya afya inayozingatia ubora na uwiano wa kijiografia inayowezesha wananchi kuzifikia na kumudu gharama za matibabu.

Aidha, katika kutekeleza lengo hilo lililosainiwa na wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Septemba 23, New York, Marekani, kama azimio la kisiasa la serikali hizo, Samia amesema nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kupitia mikakati yake na ya kimataifa, zinapaswa kuweka nguvu ya pamoja kuimarisha afya za wananchi wake kama msingi wa maendeleo endelevu.

Makamu wa Rais alisema: “Kwenye suala la kufikia lengo la afya kwa wote (UHC), Serikali ya Tanzania imeweka kipaumbele katika kuimarisha miundombinu na mifumo ya afya hususan kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa kuzingatia ubora na uwiano wa kijiografia.

Alisema pia kuwa Serikali inazingatia kuweka mifumo madhubuti inayowawezesha wananchi kumudu gharama za matibabu ambapo katika kipindi cha miaka minne (2016-2019), imefanikisha kuongeza ujenzi wa vituo vipya vya afya 352 ngazi ya kata, hospitali 67 ngazi ya wilaya na hospitali sita za rufaa kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma za afya.

Akifafanua zaidi mafanikio ya Tanzania kwenye sekta ya afya hasa katika kudhibiti magonjwa; malaria, Kifua Kikuu (TB) na Ukimwi, Samia alisema kwa upande wa malaria kiwango kimepungua kutoka asilimia 14.8 hadi asilimia 7.3 kwa miaka minne na idadi ya maambukizi mapya imepungua kwa asilimia 27.

Kwa upande wa Ukimwi, Makamu wa Rais alisema, “Mtakapojadili kuhusu masuala ya virusi vya Ukimwi mjue Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi mapya kwa kiwango cha asilimia 20.6 kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 kwa wenye umri wa miaka 15 na asilimia 31.3 kwa walio chini ya umri huo”.

Samia aliongeza; “Katika kutathimini malengo ya kimataifa ya kufikia 90-90-90, utafiti uliofanyika mwaka 2016 unaonesha kuwa, katika 90 ya kwanza inayohusu kiwango cha watu wenye VVU wanaotambua hali yaom imefikia asilimia 61 na kwa Septemba, mwaka huu imeongezeka hadi asilimia 77.2 na imevuka lengo la watumiani wa ARV kufikia asilimia 98 kwa 90 ya pili na ya tatu asilimia 88 ya wanaotumia dawa wamefubaza VVU”.

Alisema Tanzania imeweka mikakati ya kuhakikisha malengo ya 90 ya kwanza yaliobaki asilimia 12.8 yanafikiwa ifikapo 2020 na moja ya mikakati hiyo ni kufanyia marekebisho Sheria ya Kujikinga na Kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2008 yanayopendekeza kupunguza umri wa kupima VVU kutoka miaka 18 hadi 15 ili vijana wengi wapime na kuruhusu watu kujipima wenyewe VVU.

Kuhusu TB, Samia alisema, Samia alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi saba duniani zilizofikia malengo ya mkakati wa kutokomeza TB ifikapo mwaka 2020 na hadi kufikia Septemba mwaka huu vituo 10 vinatoa huduma ya tiba ya TB sugu kutoka kituo kimoja mwaka 2015.

Alisema ili kufikia malengo ya kutokomeza malaria, TB na Ukimwi kwa nchi za SADC, mkutano huo wa mawaziri wa sekta ya afya wenye kauli mbiu isemayo; Ushirikiano wan chi za SADC ni nguzo kuu kufikia maendeleo endelevu ya sekta ya afya na mapambano dhidi ya Ukimwi, unapaswa kupitia na kujadili mapendekezo ya wataalamu wa sekta hiyo na kuyafikisha kwa marais wa nchi hizo chini ya Mwenyekiti wake, Dk John Magufuli, ili kuyatekeleza mara moja.

Awali, Katibu Mkuu wa SADC, Dk Stergomena Tax, aliipongeza Tanzania kuwa kati ya nchi chache za SADC zinazofanya vizuri katika sekta ya afya hasa mapambano dhidi ya malaria na kuzitaka nchi za jumuiya hiyo kuweka kipaumbele katika sekta hiyo kwa kuanzisha mifuko ya fedha na rasilimali watu katika upatikanaji wa tiba, dawa, vitendea kazi na miundombinu ili malengo ya jumuiya hiyo yafikiwe. Dk Tax alitaka SADC kupunguza utegemezi wa fedha za wafadhili lakini

WATOTO 84,625 waliokuwa na utapiamlo mkali, wametibiwa kuanzia mwanzoni mwa ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi