loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

LIGI YA MABINGWA ULAYA Vigogo Juventus, Bayern, PSG moto chini

MECHI za raundi ya nne za michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya zimefanyika wiki hii na kutoa mwelekeo wa hatua ya kwanza ya mtoano ambayo itahusisha jumla ya timu 16.

Kwa sasa jumla ya timu 32 zinachuana katika makundi manane, huku kila kundi likiwa na timu nne, ambapo mbili za juu kutoka kila kundi ndizo zitafuzu kucheza hatua hiyo ua 16 bora. Mshindi wa michuano hiyo msimu huu wa mwaka 2019/20, ataondoka na kitita cha Euro milioni 4 (sawa na zaidi ya Sh bilioni 10). TIMU ZILIZOPENYA Tayari kuna timu ambazo zimeshajihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ya 16 bora baada ya kuwa na uhakika wa kumaliza katika nafasi ya kwanza au ya pili, kutokana na pointi walizojikusanyia.

Timu hizo ni pamoja na mabingwa wa Italia, Ujerumani na Ufaransa ambazo ni Juventus, Bayern Munich na PSG tayari zina uhakika wa kucheza hatua hiyo wakati zikisubiri kujua itamaliza katika nafasi ya kwanza au ya pili.

Juventus ya Italia, wenyewe walijihakikishia nafasi hiyo baada ya Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Russia ya Lokomotiv Moscow, wakati Paris Saint-Germain (PSG) na Bayern Munich nazo ziliungana na mabingwa hao wa Italia kucheza 16 bora.

MABAO YA USHINDI

Bao la kipindi cha kwanza lililofungwa na Mauro Icardi lilitosha kabisa kuipatia PSG ushindi baada ya kuifunga Club Brugge 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes.

Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munichi wenyewe waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Olympiakos. Nao mabingwa wa Italia, Juventus walijua wazi kuwa pointi tatu kwao zilikuwa muhimu huko Russia ili iweze kufuzu kucheza hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, ambapo ndani ya dakika nne ilipata bao kupitia kwa Aaron Ramsey.

Mpira wa adhabu wa Cristiano Ronaldo ulifika kwa kipa Lokomotiv Guilherme, ambaye alijitahidi kuuokoa kwa miguu, lakini Ramsey alimpiga tobo. Hata hivyo, Aleksei Miranchuk alisawazisha bao hilo katika dakika ya 12 kwa wenyeji. Winga Mbrazili wa Juventus, Costa akitokea benchi aliifunga bao katika muda wa majeruhi na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi katika mchezo huo. “Costa ndio kwanza amerejea katika kiwango cha juu baada ya kusumbuliwa na majeraha lakini katika mchezo huo alionesha kuwa katika kiwango cha juu na uwezi wa kucheza katika eneo lolote la uwanja,” alisema kocha wa Juve, Sarri.

PSG NA BAYERN MUNICH

PSG wenyewe wametinga hatua ya 16 bora kwa msimu wa nane mfululizo, lakini pamoja na ushindi huo dhidi ya Brugge haijaongeza nafasi ya timu hiyo kucheza kwa mara ya kwanza nusu fainali tangu mwaka 1995. Kwa upande wa Bayern Munich, ambayo haina kocha baada ya kumtupia virago kocha wao, ndio ilikuwa timu ya kwanza kupenya na kutinga hatua hiyo ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Mabao yaliyoivusha timu hiyo ni yale yaliyofungwa katika dakika za mwisho na Robert Lewandowski na Ivan Perisic na kumaliza ugumu wa Olympiakos katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

“Nimefurahishwa sana na kiwango, tumetinga hatua ya 16 bora,” alisema Hansi Flick, ambaye angepewa na ukocha wa muda baada ya kutimuliwa kwa Niko Kovac Jumapili.

Kimsimamo, Bayern inaiongoza Tottenham kileleni mwa msimamo wa Kundi B kwa pointi tano, baada ya washindi wao wa msimu uliopita kuichapa Red Star Belgrade kwa mabao 4-0 huko Serbia.

MAN CITY BADO

Mabingwa wa England, Manchester City wenyewe itawabidi kuendelea kusubiri kabla ya kutinga hatua hiyo ya makundi baada ya kujikuta ikilazimishwa ya 1-1 na Atalanta katika mchezo wa Kundi C huku ikishuhudiwa beki wake wa kulia Kyle Walker akimaliza mchezo akiwa na bao. Mabingwa hao watasubiri baada ya Atalanta kupata bao la kusawazisha katika kipindi cha pili katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa San Siro.

Raheem Sterling, ambaye alifunga hat-trick wakati Man City ikishinda 5-1 wiki mbili zilizopita, lilikiweka mbele kikosi cha kocha Pep Guardiola dakika sita tu tangu kuanza kwa mchezo huo, lakini Gabriel Jesus alikosa penalti muda mfupi kabla ya mapumziko. Kipa wa Man City Ederson alibadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Claudio Bravo wakati wa mapumziko kama tahadhari wakati timu hiyo ikisubiri pambano kali la Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu.

ZAWADI ZA WASHINDI

Washindi wa msimu huu wataondoka na jumla ya euro milioni 80, huku timu zikipata fedha kila zinaposhinda mechi zake na kila zinapovuka raundi moja kwenda nyingine. Timu zote zilizofuzu hatua ya makundi, ziliondoka na kitita cha euro milioni 15, wakati zile zitakazofuzu raundi ya 16 bora kila moja itaondoka na euro milioni 9.5 wakati robo fainali ni euro milioni 10.5.

Shirikisho la Soka la Ulaya linatoa euro milioni 2.7 kwa kila mechi timu itakayoshinda na 900,000 kwa kila mechi itakayotoka sare, ikiwa timu itashinda kila mechi wakati ikienda kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, watapata euro milioni 82.2.

OFISA Masoko wa Jiji ...

foto
Mwandishi: ZURICH, Uswisi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi