loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ATCL- Hatuajiri warembo, tunaajiri wazuri

KAMPUNI ya ndege Tanzania (ATCL) imesema haijaajiri wazee kutoa huduma kwenye ndege na pia wote wanaofana kazi hiyo wana sifa za kitaaluma kwa kuwa utaratibu wa kuwapata, umezingatia matakwa ya kimataifa yanayohusiana na kazi hiyo na si urembo wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema jijini Dar es Salaam kuwa, kimsingi wahudumu wa ndege hizo, wameajiriwa kutokana na sifa sambamba na kuwa na viwango vinavyotambuliwa na Mamlaka ya Usalama Anga (TCAA).

Amesema, ATCL ina wahudumu wa kike na wa kiume, na wote urefu wao haupungui futi 5.2 na kwamba urefu huo ni kwa mujibu wa sheria, kanuni na aina ya ndege zao na kwa kuzingatia sheria za kimataifa.

Kwa mujibu wa Matindi kuhudumia ndani ya ndege ni taaluma yenye vigezo na masharti na kwamba, ATCL inazingatia hilo

"Kwa hiyo tunapozungumzia uzuri ni ule uwezo wa kufanya ile kazi, kwangu ndiyo definition (maana) ya uzuri, uwezo wa kufanya ile kazi na ile haiba ambayo tumeieleza sie, urefu wa chini futi 5.2, uzito upo umeelezwa kabisa body mass index yaani uwiano wa urefu na uzito wa mtu, upo umeelekezwa na hii ni kwa sababu aweze kufanya kazi zake bila matatizo sio awe aende akafanye catwalk, siajiri catwalkers, hapana." amesema Matindi

Alisema ATCL inatekeleza Mkataba wa Kimataifa wa Chicago, unaoelezea viwango mbalimbali wanavyohitajika kuwa navyo watoaji wa huduma za ndege, huku ikizingatia viwango vya urefu vya wahudumu hao na mafunzo waliyopata tayari, kukabiliana na hali yoyote inayoweza kujitokeza wakati wa safari.

“Mhudumu anayepaswa kufanya kazi hizi, kwanza anapaswa kuwa mwenye uwezo wa kumiliki vifaa vyote vya usalama ndani ya ndege mbali na uzoefu wa kuogelea, kwa kuwa jukumu lake ni kuhakikisha anamsaidia msafiri kwa hali yoyote pale majanga yanapotokea,” alisema Matindi.

Kauli ya Mkurugenzi huyo, imekuja siku chache tangu kutolewa hoja na mmoja wa wabunge bungeni, aliyesema kuwa wahudumu wa ndani ya ndege za kampuni ya ATCL, hawana mvuto kutokana na kutokuwa warembo, ikilinganishwa na mashirika mengine ya ndege na hivyo kuzua mjadala.

"Tuna experienced cabin crew na lazima uwe na experience hiyo, unajua kutengeneza hao mabinti wazielewe kazi, kuwe na nidhamu kwenye ndege na kila kitu kwa hiyo ni taaluma, ni taaluma yenye masharti na vigezo, kuna kigezo cha uzuri kinazungumzwa, mimi uzuri siwezi nikau-define, sijui nyie waandishi kama mnajua, nani mzuri kati yenu hapa ajitokeze aseme uzuri ni mimi, ukitaka kuajiri ukisema uzuri ni mimi"amesema Matindi.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye alitoa ufafanuzi kwa mbunge huyo, kwa kueleza kuwa suala la wahudumu wanaohitajika kufanya kazi katika ndege hizo, linasimamiwa zaidi na taaluma na siyo urembo wao.

Akisisitiza majibu hayo, Mkurugenzi huyo wa ATCL alisema kama mahitaji ya wahudumu wa ndege hizo, yangekuwa yanahusu urembo wao, wangeweza kuwaajiri washiriki wa mashindano ya urembo, kufanya kazi katika ndege hizo.

Lakini, siyo hivyo, ndiyo maana wamewaajiri wahudumu wenye vigezo vinavyotambuliwa kimataifa.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alisema tangu kuanzishwa kwa safari za ndege kwenda mkoani Katavi, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa abiria na kuifanya ndege hiyo inayofanya safari mara moja kwa wiki kujaa kila wakati.

Alisema kutokana na hatua hiyo, wanatarajia kuongeza safari za ndege hiyo ifikapo Desemba mwaka huu baada ya kuwasili kwa ndege zingine mbili kati ya mwezi huu na Desemba.

WAKULIMA wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuchangamkia fursa ya  miche ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi