loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali ya JPM yaanzisha viwanda 17 vya nyama

MAFANIKIO katika sekta ya mifugo kwa mikaa minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, yamejidhihirisha wazi kwa kuanzisha viwanda vipya 17 vya kusindika nyama na mazao mengine ya mifugo na kufanya idadi kufikia 99 nchini.

Aidha wastani wa uwezo wa kusindika maziwa, umeongezeka kutoka lita 167,620 kwa siku hadi lita 194,335 kwa siku.

Taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015-2020 kwa kipindi cha miaka minne, iliyotolewa Septemba mwaka huu mjini Dodoma, ilieleza hayo.

Wizara hiyo ilieleza kuwa katika kipindi cha miaka minne, mafanikio hayo kwa upande wa viwanda vya nyama yamefikiwa kwa ushirikiano mkubwa wa sekta binafsi.

Ilieleza kuwa uhamasishaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi, umewezesha kuanzisha viwanda hivyo vipya vya nyama na mazao mengine yatokanayo na mifugo ikiwemo jibini na ngozi hususan katika maeneo yenye mifugo mingi ili kuongeza thamani.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa, viwanda vya ngozi vipo 13 lakini vinavyofanya kazi ni tisa huku vinavyosindika ngozi hadi hatua ya kati ni vitano na kati yake kimoja kinazalisha mpaka hatua ya mwisho na vingine vinazalisha bidhaa mbalimbali za ngozi .

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, usindikaji wa ngozi hatua ya kati umefikia futi 124,420,000 za mraba za ngozi kwa mwaka. Viwanda vya kusindika nyama nchini vimeongezeka kutoka 25 hadi 33 sawa na ongezeko la viwanda vinane.

Viwanda vilivyoongezeka ni Mitoboto Farms Ltd (Kibaha) chenye uwezo wa kuchinja na kuchakata kuku 3,000 kwa siku, Brich Company Ltd (Ubungo) nguruwe 20 kwa siku na Huacheng International Ltd (Dodoma) punda 40 kwa siku.

Vingine ni Buibui Investment Ltd (Kibaha) mbuni watano kwa siku, Meat King Ltd (Moshono Arusha) nguruwe watatu na ng’ombe saba kwa siku, Zheng He International (T) Ltd Temeke tani 3.3 za nyama ya ng’ombe kwa siku, Fang Hua Investment Co Ltd cha Shinyanga punda 40 kwa siku na GES Company Ltd Kinondoni tani nane za nyama kwa siku.

Viwanda vya kusindika vyakula vya mifugo nchini nvimefikia 94,” ilieleza taarifa hiyo

KATIBU Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora, amewaomba wamiliki ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi