loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kuongeza uwekezaji kilimo cha miwa

SERIKALI imejizatiti kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa ukienda sanjari na ujenzi wa viwanda vya sukari, kupunguza nakisi iliyopo.

Akizungumza na Habarileo hivi karibuni, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha viwanda vilivyopo vinaongeza uzalishaji wa sukari na kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa.

Mwaka jana, Rais John Magufuli alipokutana na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, aliwataka kuwekeza zaidi katika viwanda vya sukari, kukabili nakisi inayosababisha nchi kuagiza sukari kutoka nje.

Rais Magufuli alisema mahitaji ya sukari ni tani 590,000 kwa mwaka huku tani 455,000 zikiwa ni sukari ya kula na 135,000 ya viwandani. Upo upungufu wa tani 125,000 wa sukari ya kula na tani 135,000 ya viwandani.

Alitaja Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwamba ina mkakati mkubwa wa miaka mitatu wa kuongeza uzalishaji wa miwa mara mbili.

“Sasa wanazalisha zaidi ya tani 130,000 na wamesema wana uwezo wa kuzalisha hadi tani 250. Wanataka kupanua mashamba na wazalishaji wa nje wa miwa waongeze uzalishaji,” alisema.

Viwanda vya Kagera na Mtibwa pia vinatajwa kuwa na mpango wa kupanua uzalishaji wa miwa. Kwa upande wa TPC Moshi, Hasunga alisema wanashindwa kufanya upanuzi kwa sababu ya eneo kuwa dogo.

Waziri Hasunga alitaja miradi mipya ambayo serikali inaiwekea mkazo ni Mkulazi 1 na Mkulazi 2 mkoani Morogoro.

Mmoja una uwezo wa kuzalisha tani 50,000 za sukari na mwingine tani 200,000 hadi 250,000.

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia kampuni yake ya Mkulazi Holding na Jeshi la Magereza, ndiyo imeanzisha kiwanda katika Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.

“Kwa sasa hivi wameshapanda miwa maeneo mengi na walioko nje wamepata miwa mingi, kinachosubiriwa sasa ni viwanda vitakavyosindika hiyo miwa,” alisema

Alitaja kampuni nyingine ya miwa ya Morogoro, ambayo pia imewekeza katika kilimo cha miwa kwa wingi ianze uzalishaji . Ingawa alisema siyo mzalishaji mkubwa, lakini alisema itachangia uzalishaji wa sukari.

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Musa ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi