loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Changamoto za uwekezaji zipatiwe ufumbuzi

KITUO cha Uwekezaji Nchini (TIC) kinajitahidi sana kuboresha shughuli za uwekezaji nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Geofrey Mwambe, miradi 11,509 ilisajiliwa na kituo hicho katika kipindi cha kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2018.

Miradi hiyo ipo katika sekta za kilimo, maliasili, viwanda, petroli, madini, majengo ya biashara, usafirishaji, huduma, kompyuta, taasisi za kifedha, simu, mawasiliano, raslimaliwatu, miundombinu na utangazaji.

Mwambe anataja nchi zinazoongoza kwa uwekezaji katika kipindi cha kati ya mwaka 1990 hadi Desemba mwaka jana kuwa ni China, Uingereza, Marekani, Mauritius, India, Australia, Kenya, Uholanzi, Ubelgiji na Misri. Kwamba miradi yote ya uwekezaji imetoa ajira kwa watu 549,770 na ina thamani ya dola za Marekani milioni 29,120.36.

Hivyo, tunapongeza kikao kilichofanyika wiki iliyopita kati ya TIC na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), jijini Dodoma, kwa sababu kilijadili mambo mengi kwa kina, ikiwemo Mwambe alitaja changamoto tisa za uwekezaji zilizopo nchini.

Mwamba anafafanua kuwa changamoto mojawapo ni mabadiliko ya mara kwa mara ya vivutio vya uwekezaji nchini na pia mlolongo mrefu wa uhaulishaji wa ardhi na ukosefu wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji.

Changamoto nyingine ni ukosefu wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na uandaaji wa hati ndogo kwenye hati isiyo halisi.

Changamoto nyingine kuwa ni urasimu katika utoaji wa huduma kwa wawekezaji, upungufu wa Sera ya Uwekezaji ya mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997.

Pia uhaba wa miundombinu muhimu kwa ajili ya uwekezaji na uchache wa watumishi na raslimali za kufanikisha uwekezaji nchini.

Tunaunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na Mwambe kwa wabunge hao, kama vile vivutio vya uwekezaji viwekwe ndani ya sheria ya uwekezaji ili kuepuka mabadiliko ya mara kwa mara ya vivutio hivyo, ambavyo hubadilishwa na Sheria ya Fedha.

Pia, Sheria ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya mwaka 2014, itoe misamaha ya VAT kwa wawekezaji wenye mikataba na Serikali na wale ambao walikuwa wamepewa cheti cha uwekezaji na TIC kabla ya kutungwa sheria.

Hali kadhalika, kituo hicho kipatiwe bajeti kwa ajili ya akiba ya ardhi ili ziweze kutumika kutenga maeneo ya uwekezaji na kuweka miundombinu ya msingi kama vile maji na umeme.

Pendekezo lingine ni Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999, ifanyiwe marekebisho ili kuruhusu kutengeneza hati ndogo kutoka kwenye hati isiyo halisi, ili iwe rahisi kwa wawekezaji wanaojenga kwa ajili ya kuuza.

HATIMAYE safari za ndege kati ya Tanzania na Kenya zimerejea ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi