loader
Dstv Habarileo  Mobile
Simulizi za Makongoro zawacha hoi Wasanii

Simulizi za Makongoro zawacha hoi Wasanii

WAKATI wasanii wakiandaa tamasha la kumkumbuka Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, mtoto wake, Makongoro Nyerere amewaeleza wasanii jinsi alivyoshiriki vita kati ya Tanzania na Kagera, wakati baba yake hajui alipo.

Alisema hayo baada ya viongozi wa mashirikisho ya wasanii walipotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, eneo la Msasani jijini Dar es Salaam. Shirikisho hizo ni pamoja na upande wa sanaa za maonesho,ufundi,muziki na filamu.

Wasanii hao walifika nyumbani hapo kwa lengo la kuishukuru familia ya Nyerere kwa mchango mkubwa wa Baba wa Taifa aliouonesha kwa taifa na Afrika kwa ujumla, ikiwemo kutumia wasanii katika harakati mbalimbali. Akizungumza, Makongoro alianza kwa kuwauliza wasanii hao iwapo wangependa kusikia ratiba ya kila siku ya Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake,na walipoitika kwa furaha na nderemo ndipo alipoanza kueleza.

Kuhusu kwenda vitani, Makongoro alisema alishiriki kama kijana kutoka katika makundi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na akiwa nchini Uganda alipata nafasi ya kuwasiliana kwa njia ya simu na ndugu zake nyumbani, bila baba yake ( Nyerere) kukumbuka alikokuwa.

Hata hivyo alisema wakati akiendelea kuwasiliana na ndugu zake, ambao walikuwa wakigombania kupokea simu katika muda ambao baba yake alikuwa amesharudi nyumbani akitokea Ikulu ndipo alipouliza kila siku mnazungumza na nani na kwa nini mnagombea simu.

“Ndugu zangu walimjibu kuwa wanazungumza na kaka Makongoro, ambapo aliuliza kwani yuko wapi, huku ndugu zangu wakishangaa walimjibu yuko Kampala na kisha kuuliza anafanya nini huko, kesho akipiga simu nipeni nizungumze naye,” alisema Makongoro huku wasanii wakishangilia kwa utendaji wa Mwalimu Nyerere.

Makongoro aliongeza kuwa kesho yake alivyopiga simu aliisikia sauti ya baba yake katika simu (Mwalimu Nyerere), ambapo alimuuliza unafanya nini huko na Makongoro alimjibu, lakini hakumalizia kueleza kilichoendelea.

Kuhusu ratiba ya siku nzima kwa wakati wa uhai wake, alisema alikuwa akiamka alfajiri mapema akifanya mazoezi, huku akienda kanisani kwa ajili ya kusali kila siku kabla ya kwenda ofisini ambapo ilikuwa ni Ikulu.

Alisema jambo kubwa alilojifunza kwa baba yake ni pamoja na kujali muda, lakini pia kufanya maamuzi yakishirikisha pande mbalimbali na kwa makubaliano. Kuhusu wasanii hao, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba alisema walikwenda nyumbani kwa mwalimu kwa ajili ya kushukuru mchango wa Mwalimu Nyerere kwa tasnia ya sanaa nchini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6895ca7330d538ddbaf231a1575bfdef.jpg

BAADA ya kulazimishwa sare na timu ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi