loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Aussems akiri Ligi Kuu ngumu

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba SC, Patrick Aussems amekiri Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu inaushindani mkubwa kutokana na timu nyingi kupata matokeo nje ya viwanja vyao vya nyumbani.

Aidha, kocha huyo ameivulia kofia timu ya Tanzania Prisons inayoshikilia rekodi ya kutofungwa hadi sasa ikifikisha mchezo wa raundi ya 10 kwa kuwa na ukuta imara na kwamba toka ameanza kukinoa kikosi cha Simba kwenye Ligi hiyo, hajawahi kukutana na timu kama hiyo iliyoizuia Simba kuondoka na pointi tatu.

Aussems ametoa kauli hiyo baada ya kukiongoza kikosi cha Simba kwenye michezo tisa akishinda mechi saba akipoteza mchezo mmoja dhidi ya Mwadui FC, na kutoka sare dhidi ya Prisons na kufikisha pointi 22 zinazowafanya kuendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo. Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya mabao baada ya kulingana pointi na Mtibwa Sugar iliyopo katika nafasi ya pili.

Alisema kitendo cha kwao kudondosha pointi tano katika mbio za ubingwa ni pengo kubwa ambalo linavuruga malengo yao, hivyo amekiri ugumu wa ligi hiyo msimu huu. Aussems alisema upinzani unaotokea msimu huu ni tofauti na msimu uliopita, kwani kipindi kama hiki kinara wa ligi hiyo Yanga alikuwa anaongoza kwa pointi nyingi ikiwa ni tofauti na anayefuatia.

“Ligi ya msimu huu inaushindani mkubwa kutokana na timu nyingi kuwa na muendelezo chanya wa kupata matokeo nje ya viwanja vyao vya nyumbani” alisema Aussems.

Alisema pamoja na timu yake kuongoza ligi hiyo kwa sasa bado wapo kwenye presha kubwa ya kuendelea kutafuta matokeo chanya katika michezo iliyombele yao ili kulinda walichonacho na kutimiza shabaha yao ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Aussems katika kipindi hiki cha wiki mbili ambacho ligi hiyo imesimama kwa muda kupisha michezo ya kimataifa ya Taifa Stars, kwa wachezaji ambao wamebaki kwenye kikosi hicho amekiri wataendelea kufanya mazoezi mepesi kujiwinda na mchezo wao wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kupigwa Novemba 24 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

TIMU ya soka ya Polisi Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu ya ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi