loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hata wembamba hupata kisukari endapo…

Zamu yangu inafi ka. Naitwa jina. Mtaalaamu wa lishe na vyakula ananipima ili kujua urefu, unene na uzito wangu. Nina umri wa miaka 42, mama wa watoto wanne ninayejishughulisha na uandishi wa habari katika jiji la Delhi, nchini India, moja ya majiji yanayoongoza duniani kwa kuchafuka kwa hewa yake kutokana na moshi wa magari na utaokao viwandani.

Mimi hupendelea kula vyakula kama nyama na vitafunio. Kimsingi nimekuwa mara zote nikijiona mwembamba na mwenye nguvu, hasa nikijilinganisha na wanawake wa Kimarekani ambao naona picha zao kwenye Facebook. Kwa ujumla viwiliwili vyao ni mara mbili ya kile cha kwangu.

“Una urefu wa sm 87 (nchi 34.25),” anasema Chaya Ranasinghe, mtaalamu wa kituo cha Taifa cha Lishe na Kisukari cha Sri Lanka baada ya kunipima.

Niko hapa, Sri Lanka kujua kwa nini watu wenye miili midogo wa India na Sri Lanka nikiwemo mimi wanazidi kuathirika na ugonjwa wa kisukari (hususani aina ya pili), ugonjwa ambao kwa muda mrefu iliaminika kwamba ni wa watu wanene.

“Sawa, lakini kwa jinsi ulivyo ilitakuwa uwe na wastani wa urefu wa sm 80 (nchi 31.5),” anasema mtaalamu Chaya.

“Umezidi kwa sm 7 (nchi 2.75).” Chaya anachokifanya ni kunisaidia kujua kama niko katika hatari ya kuugua kisukari na upimaji wa urefu na unene wa mtu, hususani kiuno ni mambo muhimu kwa watu wenye asili ya Asia kama mimi.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba jeni (genes) za raia wengi wa Asia huonesha kwamba miili yao hutunza mafuta chini ya tumbo. Ni kutokana na mafuta haya kwenye tumbo na yaliyoko ndani ya ini yanayoelezwa na watalaamu kwamba ndio yanayotuweka katika hatari ya kuugua kisukari.

Mafuta, kwa mujibu Chanya, hufanya tishu za mwili kuwa sugu kwa insulini, homoni ambayo inarekebisha sukari kwenye damu, hivyo usukari (glucose) hujengeka kwenye damu, hatimaye kusababisha aina ya pili ya kisukari.

Kulingana na baadhi ya watafiti, Waasia na hata waafirika, kutegemeana na vyakula wanavyokula, si tu kwamba wanakuwa na mafuta mengi kwenye tumbo, lakini pia huwa na misuli michache katika eneo hilo, hali ambayo inaongeza usugu wa insulini.

Aidha, wanawake wa Asia wako pia katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari wakati wa ujauzito, hali ambayo inaweza kuwaweka watoto wao katika hatari ya kupata aina ya pili ya kisukari katika maisha ya baadaye. Hii ni ndio maana kipimo cha kiuno kinapokuwa sm 80 (nchi 31.5) kwa wanawake wa Asia na sm 90 (nchi 35.5) kwa wanaume - ni kiashiria kizuri kwamba hawako katika hatari ya kuugua kisukari.

Mbali na kiuno, mambo mengine matano yanayoangaliwa ni: historia ya familia kama huwa na ugonjwa huo, kuvuta sigara, kunywa pombe, kufanya mazoezi, viwango vya msongo wa mawazo na dhiki.

Kwangu mimi na kwa mujibu wa mtindo wangu wa maisha inaonesha kwamba niko katika hatari ya kuugua kisukari licha ya wembamba wangu kutokana na sababu hizo tano isipokuwa moja tu, ya uvutaji sigara kwa kuwa mimi sivuti. Profesa Chandrika Wijeratne, ambaye anaendesha kituo cha kudhibiti kisukari cha NIROGI nchini Sri Lanka anasema watu wengi duniani wakuwemo waasia wana kile tunachokiita” phenotype ambacho miili inapotumia nishati, kuhifadhi ziada ya chakula katika mfumo wa mafuta.

Anasema hali inakuwa mbaya zaidi katika maisha ya sasa ambayo watu wengi, hususani wa Asia na Afrika wanakula vyakula ambavyo havina tija kwenye miili yao. Wijeyaratne anasema kipimo cha mwili (body mass index -BMI) ambacho husaidia kumweka mtu katika kundi la wastani, uzito mkubwa au unene kinatakiwa kuangaliwa upya kutegemea aina ya watu kwani Wazungu ni tofauti na Wahindi, ni tofauti pia na Wachina au Waarika.

Anasema kwa wazungu, mtu mwenye BMI iliyo kati ya 25 hadi 30 kuchukuliwa kwamba uzito wake uko juu kuliko kawaida, lakini kwa raia wa Asia anatakiwa kuwa na BMI kati ya 23 na 25 kuonekana ana uzito mkubwa na kwamba hata waafrika wengi wanaingia katika kundi hili.

“Na siyo kweli kwamba ni sukari pekee inayosababisha ugonjwa wa kisukari bali matumizi makubwa ya vyakula vya wanga,” anasema.

Wakati mtaalamu wa lishe, Chaya Ranasinghe anaponichukua katika duka la vyakula, ninaonesha matunda na mboga mboga, vitu ambayo mimi hula mara kwa mara. Lakini mara tunakutana na kitu ambacho ni hatari sana katika kusababisha ugonjwa wa kisukari kwa watu wengi wa Asia (na Afrika), mchele, ambao ni chakula chao cha takribani kila siku.

Ninapomwambia kuwa ulaji wa wali ni sehemu ya maisha yangu kama ilivyo kwa watu wengi wa India, ananiambia: “Ni vyema uwe unakula wali mwekundu au wa rangi ya udongo.”

Anaendelea: “Wali mweupe uliokobolewa na kuondolewa zile nyuzi nyuzi lishe zake ina maana kwamba unakula zaidi, unajaza tumbo, lakini chakula kinayeyuka haraka tumboni. Chakula hiki pia ni haraka kugeuka kuwa sukari kwenye damu yako.”

Anazidi kusisitiza kwamba pamoja na wembamba wangu, pamoja na mazoezi, nipunguze kula wali. Kisukari duniani Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonesha kwamba kuna zaidi ya watu milioni 420 wanaougua kisukari duniani kote. WHO inabainisha kuwa tatizo la ugonjwa wa kisukari linaongezeka kwa kasi katika kipindi hiki ambapo takwimu za mwaka 2007 zinaonesha kuwa kulikuwa na wagonjwa milioni 246 duniani kote.

“Ni jambo la hatari kwa sababu ugonjwa huu ni tsunami. Nchi zinazondelea barani Afrika na watu wa Asia Kusini wako katika hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huu,” anasema Wijeyaratne.

China inaelezwa kuwa ‘nyumbani kwao’ ugonjwa wa kisukari ikiwa na watu milioni 109 wanaosumbuliwa na ugonjwa huo, sawa na asilimia 10 ya Wachina wote ambao ni takribani bilioni 1.4. India inaaminika kuwa na watu milini 69 wanaougua ugonjwa huo, sawa na asilimia 9 ya Wahindi wote. Nchini Sri Lanka, asilimia 10 wana ugonjwa wa kisukari kama ilivyo China na wengine asilimia 10 wanaonesha dalili za kuugua ugonjwa huo, hivyo jumla ya watu milioni nne katika taifa hili ambalo lina matunda ya kutosha na chakula cha bahari watakuwa wanaugua kisukari.

Tatizo kubwa la watu wa Sri Lanka kama ilivyo kwa Afrika, Tanzania ikiwemo linatajwa ni ‘kulea’ uzito mkubwa kuliko inavyostahili Kisukari nini? Kisukari ni ugonjwa ambao humpata mtu pale kongosho lake linaposhindwa kuzalisha insulini ya kutosha, au pale mwili unaposhindwa kutumia ipasavyo insulini inayozalishwa.

Hali hii husabanisha kuongezeka kwa sukari (glucose) kwenye damu (hyperglycaemia) Aina ya kwanza ya kisukari ni ile ambayo kunakuwa na tatizo la mwili kuzalisha insulini wakati kusukari aina ya pili ni pale mwili inapokuwa hauna uwezo wa kutumia insulini inayozalishwa sawasawa.

Kisukari hadi kwa watoto “Miaka 10 hivi iliyopita tulikuwa tunazungumzia aina ya pili ya kisukari kwa watu wazima. Lakini kwa sasa tunaona ongezeko la vijana walio katika umri wa miaka 20 wakiugua kisukari ikiwa ni pamoja na watoto wa shule wenye umri wa miaka 12 hadi 18,” anasema Dk Manilka Sumanatilleke, daktari bingwa wa kisukari mjini Sri Lanka.

“Hapa katika hospitali yetu ninaona vijana wadogo kati ya mmoja hadi wawili wanakuja na tatizo la kisukari kila mwezi.”

Anaelekeza lawama zake katika matumizi ya wali mweupe, matumizi ya mafuta ya nazi kwa wingi na mikate inayotokana na unga uliokobolewa. “Watu wengi wanapenda hiki chakula lakini ni hatari kwa afya zao,” anasema.

Nchi ya Sri Lanka imeanza kuchukua hatua kupambana na ongezeko linalotisha la wagonjwa wa kisukari kwa kutoa elimu ya mara kwa mara kuhusu vyakula na umuhimu wa kufanya mazoezi ili kupunguza uzito. Katika hospitali ya Taifa iliyoko Colombo, Profesa Mandika Wijeyaratne anasema kwamba hushuhudia watu wengi wakitumia pesa nyingi katika kupambana na ugonjwa wa kisukari lakini wangechukua hatua mapema wangeliokoa pesa hizo.

Anasema kuna ongezeko pia la watu ambao wanalazimika kukatwa mikono au miguu kutokana na kisukari ambacho hakikutibiwa kwa muda mrefu na kuleta athari katika mishipa ya damu na hasa wagonjwa hao wanapopata majeraha.

Kisukari pia kisipotibiwa huweza kusababisha upofu, matatizo kenye figo, magonjwa ya moyo na hata kifo. Ninaporejea Delhi, India, huku nikijua kwamba niko katika hatari ya kuugua kisukari licha ya wembamba wangu, ninaamua kubadilika. Kwa miezi mingi sasa sijala wali mweupe.

Nimeamua kula zaidi wali mwekundu. Nimeamua pia kufanya mazoezi mara kwa mara licha ya jiji hili kukosa maeneo mazuri ya kufanyia mazoezi. Ukweli ni kwamba huko nyuma, mazoezi niliokuwa ninafanya labda ni ya kutembea hatua 10 kutoka kwangu hadi ofisini kwangu ambako nikifika nakaa muda nwingi nikihariri mahojiano ya kipindi cha redio na ninapotoka kwenda nje ya ofisi mara nyingi ni kwa kuitumia gari. Lakini sasa sehemu za karibu ninatembea kwa miguu na ninapanga kununua baiskeli niwe naendesha hasa nyakati za jioni baada ya kazi.

HUDUMA bora za afya ya msingi zinapunguza uhitaji, gharama na ...

foto
Mwandishi: Hamisi Kibari

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi