loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taifa Stars yang’ara

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana ilianza vizuri mbio zakusaka nafasi ya kucheza kwa mara ya pili mfululizo fainali za Michunao ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2021 baada ya kuifunga Guinea ya Ikweta kwa mabao 2-1.

Mchezo huo wa Kundi J ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, huku wageni wakiwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililopigwa kwa shuti kali katika dakika ya 14 na Pedro akiwa nje ya meta 18. Taifa Stars baada ya kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao hil moja, lilibadilika kimchezo na kusawazisha kupitia kwa Simon Msuva aliyefanya juhudi binafsi kupata bao hilo.

Msuva kwanza, alipiga mpira wa kichwa uliogonga mwamba kabla ya kuusindikiza tena wavuni kwa mguu, katika dakika ya 68 na kuibua furaha kwa mashabiki, ambao baadhi yao walianza kukata tamaa baada ya Stars kutangulia kufungwa.

Taifa Stars ambayo mwaka huu ilishiriki kwa mara ya kwanza fainali za Afcom 2019 zilizofanyika nchini Misri baada ya miaka 39 iliposhiriki kwa mara ya mwisho mwaka 1980, ilipata bao lake la ushindi katika muda wa majeruhi, lililoihakikishia kuondoka na pointi zote tatu.

Bao hilo lilifungwa na Salum Aboubakar katika dakika ya pili ya nyongeza (dakika ya 92), baada ya mwamuzi wa akiba kuongeza dakika nne, ambapo mfungaji alipiga shuti kali lililojaa wavuni katika nyavu ndogo na kuibua furaha kwa mashabiki waliojitokesa kuishangilia timu hiyo.

Fainali hizo za Mataifa ya Afrika zitafanyika mwaka 2021 nchini Cameroon, hivyo Taifa Stars inapambana kuhakikisha inafuzu kwa mara ya pili mfululizo. Taifa Stars sasa ina kocha wa kudumu, Ettiene Ndayiragije ambaye awali alikuwa akiifundisha timu hiyo kwa muda akichukua mikoba ya Mnigeria, Emmanuel Amonike aliyetimuliwa baada ya timu hiyo kufanya vibaya katika Afcon 2019 Misri.

Taifa Stars ilipoteza mechi zake zote katika fainali hizo na kumaliza ya mwisho katika hatua ya makundi. Baada ya mchezo huo, Taifa Stars sasa inakwenda Tunisia kucheza dhidi ya Libya Novemba 19 katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Stade Mustapha Ben Jannet. Kikosi kilichoanza Stars; Juma Kaseja, Ramdahani Kessy, Mohamed Hussein, Kelvin Yondan, Bakari Nondo, Erasto Nyoni, Salum Abubakary, Mzamiru Yassin, Simon Msuva na Farid Mussa.

LIGI Kuu Soka ya Wanawake inaendelea leo ikiwakutanisha wakina dada ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi