loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ligi Kuu Bara yaacha majeraha kwa makocha

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikisimama kwa wiki mbili kupisha mashindano ya kimataifa, uwepo wa ushindani mkali msimu huu tofauti na huko nyuma ni moja ya mambo yanayozungumzwa zaidi.

Hadi sasa ligi hiyo ipo kwenye raundi ya 10 lakini utofauti uliopo kinara wa ligi hiyo Simba SC anayeongoza kwa pointi 22 amepishana kwa tofauti ya pointi mbili tu na Kagera Sugar iliyopo katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 20. Matokeo ya kinara huyo pamoja na anayeshika nafasi ya pili bado wapo kwenye presha kubwa ya kuhitaji muendelezo wa kushinda pointi tatu ili kukaa katika nafasi nzuri, la sivyo watajikuta waondolewa.

Hali hiyo ndiyo inayonogesha na kuzidisha ushindani ikiwa ni tofauti na msimu uliopita, kwani katika hatua hiyo Yanga ilikuwa inaongoza kwa pengo kubwa la idadi ya pointi nyingi ikilinganishwa na aliyekuwa anafuatia.

KUSHINDA MECHI

Pamoja na hilo kwa msimu huu kumekuwa na wimbi kubwa la timu nyingi zinazoshiriki ligi hiyo kukusanya pointi nje ya viwanja vyao vya nyumbani ikilinganishwa na msimu uliopita, ambapo kila timu ilikuwa ikijitahidi kushinda nyumbani. Vigogo vya Simba na Yanga vyenyewe angalau pamoja na Azam vilikuwa vikijitahidi kushinda hata mechi za ugenini, tofauti na timu zingine ambazo ushindi ulikuwa nyumbani.

Ni wazi ushindani huo unatokana na kila timu kujipanga mapema kutafuta pointi zitakazowahakikishia kushika nafasi za juu kwenye msimamo kuepukana na kitendo cha kujinusuru dakika za mwisho, ikiwa ni kuepukana na panga la kushuka timu nne za ligi hiyo.

Hata kwenye upande wa mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwa ufungaji bora nako ushindani umetamalaki pamoja na mshambuliaji wa Simba kuendeleza moto wake wa kupachika mabao akifikisha mabao manane akipania kutetea kiatu hicho alichotwaa msimu uliopita bado anakabiliwa na ushindani mkali kwani wachezaji wazawa wanaocheza kwenye nafasi hiyo bado wanampa ushindani mkali.

Wachezaji hao ni ni Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Paul Nonga (Lipuli FC), Yusuph Mhilu (Kagera Sugar ), Gerlad Mdamu (Mwadui FC), Peter Mapunda (Mbeya City), na Miraji Athuman (Simba SC) wote hao kila mmoja wao akiwa amepachika mabao manne. Pamoja na ushindani huo mkali hatuwezi kuwamwagia pongezi wachezaji peke yao bali zinapaswa kuelekezwa kwenye benchi la ufundi ambalo ndilo linakuwa na kazi kubwa ya kupanga kikosi na kuweka mipango ya ushindi. Kutokana na kazi yao kuwa ngumu makala haya yanakuletea makocha saba waliong’olewa kwenye mabenchi yao ya ufundi kwa sababu kadhaa ikiwemo timu kufanya vibaya au sa- babu zingine.

MWINYI ZAHERA (YANGA)

Kocha huyo raia wa DR Congo alitimuliwa baada ya kikosi hicho kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kufanya vibaya katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Zahera alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo na kibarua chake hicho kilipangwa kufikia tamati Septemba mwakani. Lakini hata hivyo ndoa hiyo imevunjika mwanzoni mwa msimu huu baada ya kocha huyo kudumu kwa kipindi cha miezi 15, huku akikiongoza kikosi hicho kwenye michezo 75 ikiwa zile za kimashindano na zile za kirafiki akishinda 45 kufungwa 17 na sare 13. Zahera amefungishwa virago baada ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi nne za ligi hiyo akifanikiwa kushinda mechi mbili sare moja akipoteza mmoja na kufanikiwa kufunga mabao manne.

ETIENNE NDAYIRAGIJE (AZAM)

Kocha huyo raia wa Burundi alijiunga na timu Azam FC akitokea timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) alijukuta akifungishwa virago baada ya kocha huyo kupata kibarua cha kukinoa kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars. Akiwa kocha na kiongozi wa benchi la ufundi ndani ya Azam alikiongoza kikosi hicho kwenye michezo mitatu akishinda yote na kufunga idadi ya mabao matano na kufungwa bao moja. AMRI SAID (BIASHARA) Said alikuwa anakinoa kikosi cha Biashara United na sababu iliyofanya kufungishwa virago ni timu hiyo kuboronga kwenye mechi za mwanzo kabisa za Ligi Kuu, ambapo kati ya mechi nne, alipoteza tatu na kufunga bao moja na kufungwa mabao matano.

ATHUMANI BILALI (ALIANCE)

Bilali ni kocha wa kwanza kufungishwa virago katika kikosi cha Alliance, kwani dakika 90 tu zilipomalizika na kibarua chake kilikoma hapo licha ya timu yake kuambulia pointi moja baada ya kutoka sare na Mbao FC. Aliiongoza Alliance kwenye mchezo mmoja na kufanikiwa kufunga bao moja na kufungwa moja na kupata pointi moja, lakini mabosi wake walishindwa kumvumilia na kumtupia virago.

FRED MINZIRO (SINGIDA)

Alifungishwa virago Singida baada ya kikosi hicho kupata matokeo mabaya ambapo alikiongoza kwenye mechi mbili hakushinda mchezo wowote na kufungwa mechi mbili na kufungwa mabao matatu.

MALALE HAMSINI (NDANDA)

Hamsini alitimuliwa Ndanda na mlezi wa timu hiyo, Gelasius Byakanwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara baada ya kikosi hicho kuwa na mwenendo wa kukosa matokeo chanya. Alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi sita hakushinda mchezo wowote, akiambulia sare tatu, kufungwa mechi tatu, wakati huo akifungwa mbao saba.

JACKSON MAYANJA (KMC)

Mayanja raia wa Uganda amejikuta akikalia kuti kavu KMC na kung’olewa baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye mechi za ligi na zile za kimataifa licha ya timu hiyo kujiwekeza vya kutosha kwenye masuala ya kiuchumi. Mayanja alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi nane, kushinda moja, sare mbili na kufungwa mabao mitano, huku akifanikiwa kufunga mabao matano na mabao ya kufungwa nane.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi