loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bodaboda acheni utani na uhai wenu

Siku mbili zilizopita nilishuhudua ajali baina ya pikipiki na daladala katika eneo la kipunguni ambapo dereva wa bodaboda aligongwa na daladala na kujeruhiwa. Sababu ya ajali ilikuwa ni matumizi mabaya ya barabara yaliyofanywa na dereva wa bodaboda yule bila kujali usalama wa maisha yake.

Dereva huyo alikua akiendesha pikipiki yake kwa mtindo wa kuchora S barabarani huku kukiwa na magari mengine yaliyokuwa yakipita katika barabara hiyo bila kujali kama anahatarisha maisha yake ama pengine angesababisha ajali na kama hiyo haitoshi dereva huyo alikuwa akifanya mbwembwe hizo bila ya kuwa na kofia ngumu

Kama yalivyo maneno ya wahenga ‘ajizi nyumba ya njaa’ ndiyo yaliyompata kijana huyo mwendesha bodaboda baada ya mwendo mfupi alijikuta akikutana uso kwa uso na daladala aina ya coaster lilimgonga na kumtupa pembeni ya barabara na kumuacha akigagaa.

Matokeo ya ajali hiyo yalikuwa ni kijana kuvunjika mguu na kupata majeraha makubwa kichwani, Nusura ya Mungu alikuwa hai na alipata msaada wa kupelekwa hospitalini na wasamaria wema.

Najaribu kutafakari tabia za waendesha bodaboda wengi wanapokua barabarani, huwa hawana umakini hata kidogo na huona kama vile wao ndiyo wenye haki pekee na barabara wanazotumia kwani hii imeonekana ni kama mfumo ama mtindo wa maisha ya waendesha bodaboda karibu wote kushindwa kufuata sheria na kanuni za barabarani.

Pia najaribu kujiuliza huwa wanafikiria nini wanapokuwa barabarani wakati wanajua wazi kwamba wanaendesha vyombo vya moto ambavyo mwili ndiyo kizuizi cha kila kitu tofauti na gari ambalo lina bodi na vitu kama airbags ambavyo vinaweza kupunguza madhara ya ajali.

Takwimu zinaonesha kwamba vifo vilivyotokana na ajali za bodaboda katika kipindi cha miaka kumi ni zaidi ya elfu nane huku majeruhi wakiwa ni zaidi ya elfu thelathini na tano.

Hii si idadi ndogo kwa nguvu kazi ya taifa kupotea na jambo la kuogopesha sana.

Ni lazima ifike mahali waendesha bodaboda mbadilike na kuanza kutumia barabara kwa kufuata sheria na kanuni alizizowekwa ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

Kama imeshindikana kuheshimu na kutii sheria na kanuni za bararani basi ni afadhali kukumbuka kwamba miili yenu ndiyo bodi ya vyombo vyenu vya moto hivyo msifanye utani nayo, jaribuni kufikiria familia na wapendwa wenu mtakaowaacha na uchungu au mtakaowasumbua kuwatunza mtakapopata ulemavu.

SERIKALI ya Rais John Magufuli tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi