loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viwanda vyaongeza ajira 9%

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sekta ya viwanda kwa mwaka jana, imeweza kuongeza ajira kwa asilimia tisa.

Aidha, amevitaka vyuo vikuu nchini kuja na tafiti za kisayansi, ambazo zitasaidia kubadili maisha ya Watanzania na kupunguza umasikini.

Majaliwa aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akizindua Kongamano la pili kuhusu Utafiti na Maendeleo Jumuishi, lililoratibiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA).

Katika kongamano hilo, Majaliwa aliwakilishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa aliyesoma hotuba ya Waziri Mkuu.

Amesema Serikali imeweka ahadi madhubuti katika sera ya maendeleo ya viwanda, ambayo inaweza kufanikiwa na kuibadilisha nchi kufikia uchumi wa kati.

Alisema kupitia azma hiyo, zaidi ya viwanda 4,000 vimejengwa katika mikoa mbalimbali na kwa mwaka 2018 sekta ya viwanda ilitoa ajira rasmi 306,180 ikilinganishwa na ajira 280,899 mwaka 2017, hivyo kuwa na ongezeko la ajira kwa asilimia tisa.

“Tanzania ina jamii kubwa inayofanya kazi ikilinganishwa na nchi nyingine za jirani, hata hivyo, moja ya changamoto kubwa zinazotukabili ni rasilimali nyingi za asili kutotumika ipasavyo. Hiyo ndio sababu tuna fursa ndogo za ajira,” alibainisha Majaliwa kwenye hotuba yake.

Alisema wakati kuna zaidi ya Watanzania milioni 24 waliohitimu na wenye ujuzi, zaidi ya asilimia 80 kati yao wanafanya kazi katika mazingira magumu, wengine wameajiriwa kwa mikataba ya muda mfupi, huku wengi wao wakiwa kwenye tishio la ajira zao muda wowote.

Aidha, Majaliwa alihimiza vyuo na taasisi za utafiti kufanya juhudi za utafiti katika sekta ya viwanda ili ziweze kusaidia upatikanaji wa fursa za ajira kwa Watanzania wenye sifa za kuajiriwa ikiwa ni katika sekta binafsi na kujiajiri.

Majaliwa alihimiza haja ya kutumia tafiti zinazofanywa na wasomi wa vyuo vikuu na vyuo vya utafiti kubadili maisha ya Watanzania.

Alisema serikali inawaahidi kuwapa ushirikiano ili maendeleo ya tafiti yaungane na vipaumbele vya serikali na jitihada za Watanzania katika kujenga uchumi wa viwanda.

Awali, Naibu Makamu wa Chuo hicho anayeshughulikia Utawala, Profesa David Mfinanga akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa William Anangisye alisema kongamano hilo ni sehemu ya programu ya ushirikiano kati ya chuo hicho na SIDA kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, unaolenga kujenga uwezo wa kufanya tafiti.

Alisema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimepiga hatua katika maeneo mengi, yakiwemo ya tafiti na utoaji maarifa katika nyanja za kitaaluma za uhandisi, sayansi asili, sayansi ya afya, sayansi ya kilimo, sayansi ya jamii, lugha na sanaa ya ubunifu.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughukikia Utafiti, Profesa Bernadeta Killian aliishukuru SIDA kwa kufadhili mradi huo, uliofadhiliwa kwa Sh bilioni 38. Mradi huo unafikia

WAKULIMA wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuchangamkia fursa ya  miche ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi