loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nyama nyekundu, mafuta hatari tezi dume

SARATANI ya tezi dume sasa imeanza kuwa tishio kwa kuwapata vijana wa chini ya miaka 40 tofauti na ilivyozoeleka. Kwa kawaida ugonjwa huo unashambulia wanaume wenye zaidi ya miaka 45.

Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya tatizo hilo ni tabia inayozidi kukua ya ulaji wa nyama nyekundu na mafuta ya wanyama uliopitiliza.

Hata hivyo zipo sababu za vinasaba. Ugonjwa huu huwashambulia sana wanaume walio na umri wa zaidi ya miaka 40 kwa asilimia kubwa lakini kwa sasa kumeonekana viashiria vya ugonjwa huo kwa watu walio chini ya umri wa miaka 40.

Tafiti zilizofanyika na kuchapwa na mitandao mbalimbali zinaonesha kwamba kwa sasa saratani ya tezi dume si ugonjwa wa wazee tena bali umeanza kuonekana kwa vijana chini ya maiaka 40 pia zikitolea mfano wa mtoto wa miaka tisa kutoka Marekani ambaye aligundulika kuwa na ugonjwa huo.

Takwimu zinaonesha kwamba ugonjwa huo awali ulikuwa unashambulia wazee wa kuanzia miaka 65 hadi 77, lakini kadri miaka ilivyoendelea kwenda umri uliendelea kushuka mpaka kufikia miaka 45.

Hata hivyo kwa sasa imeonekana kushuka zaidi. Daktari bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Hellen Makwani kutoka Hospitali ya Ocean Road akizungumzia ugonjwa huo amesema imezoeleka kwamba ugonjwa huu unawapata sana wazee na watu wenye umri wa kuanzia miaka 45 na kuendelea, lakini kwa sasa hata walio chini ya umri wa miaka 40 wanaupata.

Amesema mpaka sasa tayari wameshapokea wagonjwa wanne walio na umri wa miaka 39 na mmoja akiwa na miaka 36, wote wakiwa wameshaanza kuumwa.

Akizungumzia sababu za kupatwa ugonjwa huo, Dk Makwani amesema ni ulaji mbaya na wakati mwingine hutokana na vinasaba.

“Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni wale ambao wanakula sana nyama nyekundu na kutumia mafuta ya wanyama kwa kiasi kikubwa, unajua tuna tabia tunaona kula vyakula vya mafuta sana ndiyo kula vizuri wakati tunajiweka kwenye hatari,”amesema.

Dk Makwani ameshauri wanaume hasa vijana bila kujali umri wajitokeze kufanya vipimo mapema na kujua wako katika usalama kiasi gani kuliko kusubiri kuona dalili za wazi ambazo zinamaanisha mgonjwa yuko katika hatua ambazo siyo nzuri.

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania anayefanya shughuli zake Marekani, Flaviana ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi