loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara yaagiza CAG achunguze matumizi bil 53.2/-

WIZARA ya Kilimo imeunda timu ya watu watano kuhakiki ulipwaji wa fedha kwa wakulima wa korosho kwa msimu wa 2018/2019 baada ya kunusa ufi sadi katika malipo hayo.

Aidha imemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kuchunguza na kuhakiki matumizi wa fedha za uliokuwa Mfuko wa Wakfu kutokana na kuwepo kwa matumizi yasiyofaa ya fedha Sh bilioni 53.2 .

Taarifa hizo mbili zinatakiwa kuwa zimekamilika ifikapo Januari 15 mwakani kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki kwa watakaobainika.

Hayo yamebainishwa jana jijini hapa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa malipo ya korosho zilizonunuliwa na Serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa mwaka 2018/2019.

Alisema mpaka mwisho wa msimu, takribani tani 222,561.2 za korosha ghafi zilikuwa zimekusanywa zikiwa na makadirio ya thamani ya Sh bilioni 723.8.

Alisema kati ya korosho hizo zilizokuwa daraja la kwanza zilikuwa tani 204,476.1 zenye thamani ya Sh 674,771,522,700 na zile za daraja la pili zilikuwa tani 18,084.9 zenye thamani ya Sh Sh 47,744,294,400.

“Hivyo kumeifanya Serikali iwe imelipa wakulima kwa korosho kwa tani 217,786 zenye thamani ya Sh bilioni 707.8.

“Azama ya serikali ilikuwa ni lazima kulipa malipo ya wakulima wote, lakini hadi leo tunapozungumza hapa, malipo ya wakulima bado hajaisha, na hii inatokana na mambo ambayo yamejitokeza kwenye malipo.”

Hasunga alisema pamoja na kuwa kamati ya ulinzi na usalama na ile ya kilimo kufanya uhakiki, wamebaini kuwapo udanganyifu mkubwa katika malipo ya wakulima.

“ Sasa kutokana na udanganyifu huo unatupa shaka kama viongozi wa wizara kwamba huenda hata baadhi ya ya wakulima waliolipwa sio sahihi.”

Hasunga alitolea mfano Chama cha Msingi cha Sangasanga AMUCOS ambacho kimefanya udanganyifu kwa kuongeza kilo zaidi ya 7,000 huku wakilipwa malipo hewa ya zaidi ya Sh milioni 222.2

Aidha alisema kuna baadhi ya watu waliolipwa sio wakulima, na ambao hawakuleta korosho kwenye chama cha msingi lakini majina yao yapo kwenye malipo ya mwisho na fedha ambazo zimelipwa kwa watu ambao sio wakulima ni Sh 222, 328, 867 na hii ni kwenye chama kimoja tu cha Sangasanga.

Alisema pia katika baadhi ya vyama uhakiki uliweza kuokoa zaidi ya Sh bilioni 1.6 ambazo zingelipwa kwa wakulima hewa.

“ Kuna vyama vingine pia tumepata changamoto kama hizo, kule Tandahimba kama isingekuwa uadilifu wa wale waliosimamia uhakiki kulikuwa na Sh bilioni 1. 6 zilikuwa zinapotea na maeneo mengine imeonekana upo udanganyifu.”

Hasunga alisema timu hiyo ya watu watano iliyoundwa inatakiwa kuhakikisha inaangalia kama korosho zilizopokelewa ndizo zilipo na ndio kiasi kilichouzwa na kama kuna upungufu ni kiasi gani.

Hasunga alisema Timu hiyo pia inatakiwa kuhakiki kama kuna wakulima ambao mpaka sasa bado hawajalipwa.

Aidha, Hasunga alisema wizara yake pia imemuagiza CAG kufanya uchunguzi na uhakiki wa matumizi ya fedha Sh bilioni 53.2 za uliokuwa Mfuko wa Wakfu ambazo zililenga kujenga viwanda vitatu, maghala na kuendeleza zao la korosho.

“Mwishoni wa mwaka 2016, serikali iliamua kufuta Mfuko a Wakfu na wakati huo kwenye akaunti ya mfuko huo kulikuwa na kiasi cha Sh bilioni 53.2 kwa ajili ya kujenga viwanda vya kubangulia korosho Mkinga mkoani Tanga, Tunduru-Ruvuma na Mkuranga-Pwani.

“ Kilichojitokeza Bodi ya Korosho badala ya kutekeleza maagizo ya serikali wakabadilisha matumizi ya fedha, viwanda havikujengwa, maghala hayakujengwa na wakatumia fedha tofauti na maagizo ya serikali

Hasunga aliongeza: “ Kilichotushtua mwaka huu wakati minada inaendelea wale walioagiza magunia kwa misimu iliyopita kwamba wanaidai serikali kiasi cha Sh bilioni 12 kwa ajili ya magunia ya msimu wa mwaka 2017/2018.

Alisema wakati huo, utaratibu uliokuwepo mnunuzi wa korosho ndiye aliyetakiwa kulipia magunia hayo.

“Swali linakuja kuwa fedha za magunia, ni kwanini hazijalipwa na leo Serikali inadaiwa?” alisema.

Alisema katika matumizi yaliyoanishwa na Bodi ya Korosho pia ilikuwa ni kuvipa Vyama Vikuu vya ushirika kulipia madeni yao ya nyuma ya benki ambako chama cha TANEKU Ltd kilipewa Sh bilioni 1.87 na chama cha CORECU kilipewa Sh bilioni 2.12.

MGOMBEA urais  wa Zanzibar aliyepitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi