loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Swahili Fashion Week Desemba 6-8

SHINDANO la ubunifuni wa mavazi maarufu Swahili Fashion Week limepangwa kufanyika Desemba 6 hadi 8, likiudhuriwa na mbunifu maarufu kutoka Italia, Marta Zampolini.

Akizungumza jana, Mratibu wa shindano hilo, Mustafa Hassanali alisema mwanamitindo huyo wa Italia atatoa mafunzo kwa wanamitindo hapa nchini namna ya kujibrand na kubrand bidhaa zao ili ziuzike nje ya nchi.

Aidha, alisema  shindano hilo litausisha wanamitindo 34 kutoka ndani na nje ya nchi  na litafanyika kwenye ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.

Alisema zoezi la kuwasaka wana mitindo wenye muonekano makini kwa ajili ya kuonyesha mitindo ya mavazi katika jukwaa la Swahili Fashion Week kwa mwaka huu, litafanyika Novemba 24.

 Vigezo ambavyo vitatazamwa   kwa wanamitindo hao ni urefu usiopungua sentimita 172 bila viatu virefu kwa wanawake na, sentimita zisizopungua 180 kwa mwanaume ikiwa ni pamoja na muonekano wa kuvutia.

Hassanali alisema pia mwaka huu kutakua na tuzo maalum kwa wabunifu kutoka mkoani ili kuwapa fursa na kuwatambulisha kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Adrian Nyangamalr alisema jukwaa la Swahili Fashion Week ni kiunganishi kwa nchi zinazoongea Kiswahili lengo likiwa ni kukiza lugha ya Kiswahili na pia kujitangaza zaidi kimataifa kuelekea uchumi wa kati.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi