loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkapa aeleza alivyoumia mabadiliko uchaguzi 2015

RAIS mstaafu Benjamin Mkapa ameelezea namna alivyoathiriwa na kusogezwa mbele kwa tarehe ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, uliomwingiza madarakani Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Mkapa ameelezea hayo kuanzia ukurasa wa 217 na 218 kwenye Sura ya 14 ya kitabu chake kiitwacho “My Life My Purpose” kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

Uchaguzi Mkuu huo ulipangwa kufanyika Oktoba 30, 2005, lakini siku tatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza kuusogeza mbele hadi Desemba 14 kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jumbe Rajab Jumbe.

Mkapa alisema, “kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, uchaguzi ni lazima usogezwe mbele angalau kwa siku 21 kama iwapo mgombea wa nafasi ya uraisi au Makamu wa Rais ataaga dunia, hivyo hiyo ilimaanisha kuwa ninapaswa kuendelea kukaa Ikulu tena kama Rais kwa muda huo.”

Alisema suala hilo lilimuumiza akili, kwa kuwa alikuwa ameshajiandaa kuondoka Ikulu na alishaanza kuondoa baadhi ya vitu muhimu katika Ikulu hiyo na kuhamishia kwenye nyumba yake ya Sea View, Upanga jijini Dar es Salaam. Alisema alikuwa ameshajiandaa kuondoka Ikulu na tayari mkoani Arusha, alishaandaliwa hafla ya kuagwa na nyingine ilikuwa mkoani Tabora na alikuwa ameshajiandaa kuhudhuria.

Akielezea alivyopata taarifa hiyo, alibainisha kuwa alikuwa ametokea kanisani kusali na ndipo siku hiyo ya Jumapili alifuatwa na Mkuu wa Ulinzi aliyemwambia kuwa “nina habari mbaya kwako mkuu” na kisha akamwelezea kuhusu kifo hicho cha Jumbe.

Alisema alishikwa na butwaa na kuuliza, “ehee Mungu kwa nini unataka kunifanyia hivi”. Alitafakari na kisha kumwagiza Mkuu huyo wa Ulinzi kuwasiliana na aliyekuwa Spika wa Bunge, Pius Msekwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, kuangalia kama kuna uwezekano wa kuendelea na uchaguzi kama kawaida.

Alisema baada ya muda, aliambiwa hakuna jinsi, zaidi ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo. “Lakini uchaguzi ulifanyika vema na kisha Rais Jakaya Kikwete akaingia madarakani, hakika niliona kuwa nimeutua mzigo na hiyo inajidhihirisha hata watu walivyokuwa wakiniaga, na mie nakiri haikuwa kazi ndogo kuongoza nchi,” alisema Mkapa.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi