loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kashfa ya rushwa yamweka pabaya Rais Trump

Kashfa ya rushwa yamweka pabaya Rais Trump

MAHOJIANO yenye lengo la kuamua mustakabali wa uwepo madarakani wa Rais Donald Trump yameendelea huku yakichukua sura mpya baada ya maofi sa kadhaa wa serikali yake kutoa ushahidi mbele ya Kamati ya Usalama unaoonekana kumweka matatani kwa kile kilichodaiwa kuwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Chanzo cha mahojiano hayo yanayoendelea mbele ya Kamati ya Usalama ilikuwa ni mazungumzo ya simu baina ya Trump na Rais wa Ukraine, Vlodymyr Zelenskyy ambayo inasemekana yalimtaka Zelenskyy kuanza uchunguzi dhidi ya Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden na mtoto wake wa kiume ambaye anafanya kazi katika bodi ya gesi ya Ukraine.

Habari zinasema kuwa Trump aliagiza uchunguzi huo kwa Biden ambaye anatazamiwa kuwa mshindani wake mkubwa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi ujao akiwa na lengo la kumdhoofisha lakini hakukuwa na kosa lolote kwa wanafamilia hao. Ilisemekana kuwa Trump alizuia kiasi cha Dola za Marekani milioni 400 kwa ajili ya jeshi la Ukraine akishinikiza uchunguzi huo ingawa baadaye zilitolewa huku Trump akikanusha uwepo wa mazingira ya rushwa katika mazungumzo yake na Zelenskyy.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Ulaya, Gordon Sondland katika ushahidi wake alisema kuwa Trump ameonesha ishara za wazi za uwepo wa ufisadi ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Sondlad alipingana na taarifa ya Trump kwamba hakukuwa na mazingira ya rushwa katika mazungumzo yake na Zelenskyy na kusema kuwa kuwa Trump alitumia madaraka yake kushawishi Ukraine kwa misaada kwa ajili ya manufaa yake binafsi katika uchaguzi ujao.

“Najua wajumbe wa kamati hii mnataka kujua kama kulikuwa na viashiria vya rushwa katika jambo hili, kama nilivyotoa ushuhuda hapo awali jibu ni ndiyo!” alisema kwa msisitizo kuonesha uhakika wa anachokizungumza.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya usalama, Adam Schiff alisema ushahidi wa Sondland ni moja ya ushahidi muhimu mpaka kufikia sasa kwani unazungumzia jambo kubwa sana kwa Rais.

“Hili ni jambo linalogusa utendaji wa Rais na uchunguzi wake unatupeleka moja kwa moja katika suala la rushwa,” alisema. Trump anakuwa Rais wa nne kuingia katika mahojiano ya namna hiyo wa kwanza akiwa Andrew Johnson mwaka 1868, Richard Nixon mwaka 1973 na Bill Clinton mwaka 1998.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f9f2cca6b3f1a6ce8aeb4352c8d6fb67.jpeg

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON DC, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi