loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Malecela- JPM anafanya kazi kubwa mno

WAZIRI Mkuu Mstaafu, John Malecela amesema kutojitokeza wagombea wa vyama vya siasa vya upinzani kugombea nafasi za wenyeviti za Serikali za Mitaa, Vitongoji na Kata katika Jimbo la Mtera kunaonesha namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojikita katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

Malecela amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Mvumi Misheni Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Amesema utendaji kazi wa Rais John Magufuli unawavutia wananchi wengi ndiyo maana wanachama wa vyama vya upinzani hawakuona sababu ya msingi kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi hizo.

Alisema serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kero zilizokuwa zikikwamisha wananchi zinatatuliwa.

“Kazi zilizofanywa na Rais Dk Magufuli ni kubwa mno kuanzia miundombinu ya barabara, shule, maji na huduma za kiafya,hivyo inatupasa kushirikiana na serikali katika kufanya kazi kwa bidii bila kuangalia itikadi yoyote ya kisiasa ili kuleta maendeleo zaidi kwa Watanzania wote,” amesema Malecela.

Aliwataka wenyeviti wa serikali ya mitaa na vitongoji watakaopitishwa kufanya kazi zao bila ubaguzi au kujali itikadi za kisiasa, dini, rangi au kabila bali wawatumikie wananchi kwa maslahi ya kuleta maendeleo ya Taifa.

Alisema wenyeviti hao wahakikishe wanafanya kazi zao bila ubaguzi pamoja na kutoangalia itikadi yoyote ya kisiasa kwa wananchi watakaowahudumia kwa kuwa wamepewa dhamana kwa ajili ya kuwatumikia watu wote.

Alisema baadhi ya maeneo viongozi waliojitokeza kugombea nafasi hizo za uenyekiti wa vitongoji, mitaa na kwenye kata kupitia CCM bila upinzani wowote ni muhimu wakaifanya kazi hiyo kwa uzalendo na kuzingatia Katiba ya nchi ikiwa na mwongozo wa chama tawala, CCM.

Waziri Mkuu huyo mstaafu pia aliwataka vijana wa Tarafa ya Mvumi kujikita katika shughuli za kilimo cha zabibu pamoja na ufugaji wa nyuki na ufugaji wa mifugo mbalimbali ikiwemo kuku, ng’ombe mbuzi na kondoo.

Alisema shughuli hizo zitawawezesha kubadilisha maisha yao kiuchumi zaidi kwa upande wao ikiwa na kwa Taifa kwa ujumla.

Aliwapongeza kinamama kwa juhudi kubwa wanazozifanya kwenye upande wa ujasiriamali ambao kwa sasa ni mkombozi katika kuleta maendeleo ndani ya familia wanazotoka.

Jimbo la Mtera lenye vijiji 60 linaongozwa na mbunge Livingstone Lusinde (Kibajaji).

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi