loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kili Stars mguu sawa Chelenji

KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars tayari kimeingia kambini kujiandaa na michuano ya kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) inayotarajiwa kuanza wiki ijayo mjini Kampala.

Kikosi hicho kilichopo chini ya kocha, Etienne Ndayiragije akisaidiwa na Selemani Matola na Juma Mgunda kilianza mazoezi jana jioni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Akizungumza jana, Matola alisema wachezaji wote 32 wameshaingia kambini na wameshaanza mazoezi hayo ya awali kujipanga kuendeleza upinzani kwenye michuano hiyo kama ilivyokawaida yao.

“Wachezaji wote tuliowaita wameshawasili kambini tangu juzi na wengine wanaotoka nje ya Dar es Salaam, waliungana na timu leo asubuhi (jana) katika programu ya awali ya mazoezi mepesi,” alisema Matola.

Matola aliongeza kwamba michuano hiyo itakuwa na upinzani mkali kutokana na timu kuonekana kufanya maandalizi ya nguvu. Michuano hiyo inatarajiwa kushirikisha timu 12 zilizopangwa kwenye makundi matatu, ambapo Kilimanjaro Stars ipo kundi C pamoja na timu za Kenya, Zanzibar na Djibouti wakati kundi A likiundwa na timu za Uganda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, na Kundi B lina timu za Congo DR, Sudan Kusini, Somalia na Sudan.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi