loader
Picha

Mahafali ya mabaharia kufanyika wiki ijayo

WAHITIMU wa kozi za weledi wa (umahiri) wa ubaharia ni miongoni mwa watakaoshiriki katika mahafali ya 15 ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi, wiki ijayo.

Kwa kujibu wa tangazo la DMI lililotolewa leo, Desemba 6, 2019, na kuchapishwa kwenye gazeti la kila siku la Kiingereza, Daily News leo, wahitimu wa chuo hicho, mabaharia wametofautishwa na wahitimu wengine kimuonekano kwa kuwa wanatakiwa kuvaa mavazi yao mahususi ya kazi (professional dressing).

“Vazi ni kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ni suruali nyeusi na shati jeupe ya mikono mifupi….” limeelekeza tangazo hilo kwa wale ambao si mabaharia.

Hata hivyo, mabaharia na wahitimu wengine wanapaswa kuthibitisha kwao kuwa watashiriki tukio hilo kabla ya Jumatatu kwani Jumanne watapaswa kupata mazoezi kwa ajili ya mahafali hayo.

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la Raleigh Tanzania linaendelea na kampeni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi