loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Masauni ataka mkakati kutokomeza udhalilishaji

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kuanzisha mkakati maalumu wenye lengo la kutokomeza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ulawiti, ubakaji.

Aidha amelitaka jeshi hilo kuhakikisha upelelezi wa kesi hizo unakamilika kwa wakati. Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha makamanda wa polisi wa mikoa mitatu ya Unguja na wakuu wa upelelezi, Masauni alisema kuna takwimu zinazoonesha kuongezeka kwa matukio hayo. Kwa mfano, Masauni alisema kwa mujibu wa takwimu mwaka huu matukio ya udhalilishaji wa kijinsia, ikiwamo ubakaji yamefikia 280.

“Matukio ya vitendo 280 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu ni vingi na juhudi za haraka za makusudi zinahitaji kuchukuliwa ili kukomesha na kupambana na matukio hayo ambayo yametia doa kubwa na aibu,” alisema.

Masauni alisema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wazazi kuhusu matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia yanayowahusisha watoto chini ya umri wa miaka 18. Kwa mfano aliwataka polisi kuwapatia mafunzo watendaji wake ambao watakuwa na uwezo na mbinu za kufuatilia kesi za udhalilishaji wa kijinsia.

Aidha alikitaka kikosi cha upelelezi kufuatilia kesi za udhalilishaji wa kijinsia kwa sababu miongoni mwa malalamiko na takwimu za kesi hizo nyingi zipo katika hatua ya upelelezi kwa muda mrefu.

“Yapo malalamiko kutoka kwa jamii na wazazi kwamba kesi za udhalilishaji, upelelezi wake unachukuwa muda mrefu sana...hili jeshi polisi tunataka mlifanyie kazi haraka,” alisema.

Mapema Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohamed Hassan Haji alikiri kuwepo kwa kasi ya matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na kuitaka jamii kutoa taarifa za matukio hayo haraka.

MTOTO Juma Megejuwa (12) mkazi wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi