loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbinga kutoa mikopo kwa wanaotaka kuanzisha viwanda

SERIKALI wilayani Mbinga imesema itatoa kipaumbele kwa waombaji wa mikopo wenye mwelekeo wa kuanzisha viwanda ili kujenga uchumi wa viwanda na kuongeza ajira wilayani humo.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye wakati wa ufunguzi wa semina ya wazalishaji, wasindikaji na wauzaji wa bidhaa za chakula na vipodozi iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga. Nshenye alisema mikopo inayotolewa na halmashauri ya wilaya kwa makundi ya vijana na wanawake haina riba, na kwa sasa watakaopewa kipaumbele ni wale ambao wameitikia wito wa kuanzisha viwanda vya kusaga kahawa, watengenezaji wa batiki, wazalishaji wa sembe na bidhaa nyingine mbalimbali.

“Walioitikia wito wa kujenga uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda tunawapongeza kwani tuna imani kuwa ajira zitaongezeka na Kauli ya Mbinga Mbinguni itazidi kujidhihirisha kutokana na mafaniko yatakayotokana na viwanda,” alisisitiza.

Mkuu huyo alisema pamoja na jitihada hizo za wazalishaji za kuanzisha viwanda, pia wazalishaji wanapaswa kuzalisha bidhaa kwa kuzingatia viwango ili kuwa na uhakika wa ubora na bidhaa wanazozizalisha pamoja na uhakika wa soko ndani na nje ya Wilaya hiyo.

Alisema fursa ya elimu inayotolewa na TBS ni muhimu kwa wazalishaji kuizingatia kwani mbali na elimu hiyo inayotolewa bure pia wajasiriamali hupatiwa huduma ya uthibitishaji wa ubora wa bidhaa bure kwa miaka mitatu ya mwanzo.

Aidha akizungumzia kundi maalumu la wasindikaji wa pombe za kienyeji Mkuu wa Wilaya ameiomba TBS kuangalia namna ya kuwawezesha wasindikaji pombe za kienyeji kufikia viwango vinavyokubalika ili bidhaa zao zikidhi matakwa ya viwango na kukubalika katika masoko ya ndani na nje ya nchi hususan katika soko la Afrika Mashariki.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora na Meneja wa Utafiti na Mafunzo, Hamisi Sudi akimkaribisha Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Dk Athuman Ngenya alisema, Shirika litaendelea kutoa elimu ya viwango kwa watanzania wote lengo kuu likiwa ni kuwa na uwelewa wa pamoja wa masuala ya viwango na ubora wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na zile zinaingizwa kutoka nje nchi.

Mkuu wa wilaya ya Songea, Palolet Mgema akifungua semina katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea alisema semina hii imefanyika katika kipindi muafaka kwani wafanyabiashara na wazalishaji walikuwa wakiisubiri kwa hamu ili kujua ni taratibu zipi za kufuatwa baada ya mabadiliko ya Sheria ya fedha ya Mwaka 2019.

Tangu Julai mwaka huu Shirika limefanya semina mbalimbali kwa wasindikaji,wazalishaji na wauzaji wa bidhaa za kilimo na chakula na vipodozi katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kigoma, Katavi na sasa mkoani Ruvuma na semina kama hii itaendelea kutolewa nchi nzima.

TAKRIBANI mifugo 12,000 katika vijiji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mbinga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi