loader
Picha

Kivumbi Cecafa wanaume leo

MICHUANO ya kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa wanaume inatarajiwa kutimua vumbi leo mjini Kampala kwa timu za kundi A, wenyeji Uganda wakitarajiwa kuchuana na Burundi na Somalia dhidi ya Djibouti.

Michuano hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Startimes jijini Kampala imeandaliwa na Baraza la soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa). Mechi za kundi B zitachezwa kesho ambapo Kilimanjaro Stars itachuana dhidi ya Kenya na Zanzibar Heroes dhidi ya Sudan. Katika michezo ya leo, wenyeji Uganda ni timu nzuri yenye wachezaji wengi vijana na wamekuwa wako moto baada ya kuonekana kufanya vizuri kwenye michezo kadhaa iliyopita ya Afrika. Na kadhalika, Burundi pia sio wabaya ni moja ya timu zenye ushindani mkubwa.

Mara ya mwisho Uganda kuchuana na Burundi katika michuano hiyo, ni mwaka 2017 walitoka suluhu. Huenda Uganda kwasababu wako kwenye kiwanja walichokizoea ikawa nafuu kwao kutowaangusha mashabiki wao. Mechi ya Somalia na Djibouti.

Timu hizo hazikushiriki mashindano yaliyopita huenda sasa wakaja na nguvu. Somalia kama watakuwa wameita wachezaji wao wanaocheza soka la kulipwa nje basi watakuwa kwenye nafasi ya kufanya vizuri. Siku za hivi karibuni walionekana kubadilika na kuonyesha soka la kiushindani tofauti na miaka iliyopita. Kwa upande wa Djibouti nao pengine watakuwa wamejiandaa kuja kushindana la sivyo, wanaweza kula kichapo kwa ndugu zao hao wa Somalia.

MABINGWA wa kihistoria Yanga kupitia Kampuni ya GSM wamesema wanajipanga ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi