loader
Picha

Mamia wamzika Tigana Dar

MWILI wa mchezaji wa soka wa zamani wa Tanzania, Ally Yusuf ‘Tigana’ umezikwa jana katika makaburi ya Msasani, Dar es Salaam na kusindikizwa na maelfu ya wadau wa soka na wachezaji wa zamani.

Tigana ambaye aliwahi kuzichezea Simba na Yanga kwa nyakati tofauti pamoja na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ alifariki juzi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Amana baada ya kuugua kwa muda mfupi. Akizungumza jana mchezaji wa zamani wa Yanga Ramadhan Kampira alisema Tigana ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa na nidhamu hivyo alikuwa rafiki wa kila mtu.

Tigana alizaliwa mwaka 1970 Ilala, Dar es Salaam na amekulia mtaa wa Saadani na kusoma shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko ambako alianzia soka akicheza kama kipa na baadaye kuwa mchezaji wa ndani.

Aliwahi kuzichezea timu za Shaurimoyo Kids, Manyema Rangers mwaka 1989 ambapo alidumu hadi 1991 na kuchukuliwa na Pan African ikiwa daraja la pili (sasa daraja la kwanza) na kuipandisha Ligi Kuu mwaka 1993.

Mwaka 1994 alisajiliwa Yanga SC, ambayo alidumu nayo kwa msimu mmoja na kuchukuliwa na watani wao Simba ambapo alidumu hadi 1997 na kwenda Cadets ya Mauritius na kucheza hadi mwaka 2000 na kurudi tena Simba.

Aliporudi Simba alicheza msimu mmoja na kurudi tena Yanga ambapo alikaa hadi mwaka 2004 na kwenda kumalizia soka lake katika timu ya Twiga ya Kinondoni. Jina la Tigana alipewa baada ya kufananishwa na kiungo wa Ufaransa, Jean Pierre Tigana miaka ya 1980.

MABINGWA wa kihistoria Yanga kupitia Kampuni ya GSM wamesema wanajipanga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi