loader
Picha

NSSF yathamini nyumba za Kigamboni ili ziuzwe

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea miradi ya nyumba za shirika hilo zilizojengwa maeneo ya Toangoma, Mtoni Kijichi na Dugu, wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio mwishoni mwa wiki iliyopita katika ziara ya miradi hiyo iliyomhusisha Mthamini Mkuu wa Serikali, Evelyne Mugasha ili kufanya uthamini wa bei ya kupangisha na kuuza nyumba hizo mwanzoni mwa Desemba.

“Tulikuwa na ujio wa Waziri Mkuu, Majaliwa akifuatana na mawaziri kadhaa kuangalia miradi ya nyumba tulizozijenga katika maeneo ya Toangoma, Mtoni Kijichi na Dungu huko Kigamboni. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kuhakikisha kwamba zile nyumba zilizokamilika ziweze ama kuuzwa au kupangishwa kwa wananchi ili kuwafanya wananchi wawe na makazi bora, lakini vile vile kutuwezesha sisi kupata mapato yanayotokana na uwekezaji huu,” alisema.

Erio aliongeza kabla ya kuuza au kupangisha inatakiwa kufanyika tathmini ya kitaalamu ili waweze kupanga bei ya kupangisha au kuuza nyumba hizo.

“Lakini kabla ya kuuza au kupangisha inatakiwa ifanyike tathmini ya kitaalamu, nyumba hizo ziuzwe au zipangishwe kwa bei gani. Tunao wataalamu ndani ya serikali wakiongozwa na mthamini mkuu wa serikali tulioelekezwa na Waziri Mkuu, tumewapata na wamefika kufanya tathmini hiyo,” alisema Erio.

Mdhamini Mkuu wa serikali, Evelyne alisema wamefika katika maeneo ya miradi hiyo ili kufanya tathmini na kutoa bei ya soko kwa nyumba hizo. “Tulipokea maelekezo tuje tufanye ukaguzi na kutoa bei ya soko ya sasa, kwa nyumba hizi zitawafanya wananchi waweze kupanga au kununua,” alisema.

ELIMU ya Awali ni sehemu muhimu sana ya dhana nzima ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi