loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mahakama yaagiza Ester Bulaya kusalimisha pasi ya kusafiria

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imemuamuru Mbunge wa Bunda Mjini, mkoa wa Mara, Ester Bulaya kuwasilisha mahakamani hapo hati yake ya kusafi ria ili aweze kuhojiwa kuhusu kesi ya uchochezi inayomkabili.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kuwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Hakimu Simba alisema hati hiyo inatakiwa kuwasilishwa mahakamani Desemba 19, mwaka huu ambapo kesi hiyo itaendelea kwa upande wa mashitaka kuuliza maswali kutokana na ushahidi wake alioutoa.

Awali, akihojiwa na Wakili Simon, Bulaya alidai alimpeleka Mbunge wa Kawe, Halima Mdee nchini Afrika Kusini baada ya kufunga mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni. Bulaya alidai alihudhuria mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Februari 16, 2018 na alipata nafasi ya kuwasalimia wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Mshitakiwa huyo wa tisa alidai kuwa kabla ya kumalizika kwa mkutano huo, aliondoka viwanjani hapo yeye na Mdee kwenda nyumbani kwao ili kujiandaa na safari ya kwenda Afrika Kusini ambako Mdee alitakiwa kwenda kupatiwa matibabu.

Kutokana na maelezo hayo, Simon aliiomba mahakama imuamuru Mbunge huyo kuwasilisha mahakamani hapo hati yake ya kusafiria na mara baada ya kuileta ndio wataendelea kumuuliza maswali baada ya kumaliza kujitetea.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 19, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji. Mbali na Bulaya na Mdee, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche. Wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washitakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

TAKRIBANI mifugo 12,000 katika vijiji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi