loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shirika lakubali kishindo cha Magufuli

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania (TEDEF), limetambua juhudi na kuthamini kazi anazofanya Rais John Magufuli, kuhakikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifi kapo 2025 inafi kiwa.

TEDEF imemtunuku tuzo Rais Magufuli na kuwa miongoni mwa watanzania 10 waliofanya vizuri kwa kutoa mchango wao kuimarisha Diplomasia ya Uchumi wa nchini. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Magufuli na kuwakabidhi tuzo hizo watanzania wengine walio mstari wa mbele kuinua diplomasia ya uchumi nchini katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam juzi. Shonza aliishukuru TEDEF kwa uamuzi wa kushirikiana na serikali katika kuimarisha diplomasia ya uchumi nchini.

“Diplomasia ya uchumi ni muhimu kwa ustawi wa taifa. Mataifa yote makubwa duniani yameipa umuhimu wa kwanza diplomasia ya uchumi ambao umekuwa ni muhimili wa kukuza mataifa hayo. TEDEF mmekuwa wazalendo kwa kutambua na kuthamini mchango wa viongozi na wananchi mbalimbali katika kuhakikisha nchi yetu inafikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati,” alisema Shonza.

Miongoni mwa kazi zilizomfanya Rais Magufuli kupewa tuzo hiyo ni mchango wake katika kujenga miundombinu ya kufanikisha diplomasia ya uchumi Tanzania, ikiwemo miradi ya Reli ya Kisasa (SGR), Kampuni ya Ndege (ATCL), ujenzi wa barabara na madaraja na mradi wa umeme wa Bwawa la Nyerere.

Watanzania wengine waliopata tuzo za kushiriki kujenga diplomasia ya uchumi ni mawaziri wawili, ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi kwa kuongoza majadiliano ya biashara ya kimataifa baina ya Tanzania na Kampuni ya Madini ya Barrick kwa mafanikio makubwa kwa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola ambaye anasimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kwa kutambua amani iliyojengeka ni muhimu kwa kufanikisha Diplomasia ya Biashara na Diplomasia ya Uchumi.

Tuzo hizo pia zimeenda kwa mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi, ambao nao wametambuliwa kwa mchango wao katika kujenga diplomasia ya uchumi, nao ni Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda ukiongozwa na Balozi Ernest Mangu ambao umeongoza kwa mauzo ya nje katika nchi za Afrika Mashariki na Ubalozi wa Tanzania nchini China, ukiongozwa na Balozi Mbelwa Kairuki kwa kuongoza katika uwekezaji mitaji nchini.

Pia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ukiongozwa na Balozi Wilson Masilingi, ambao umeongoza kwa kuleta watalii nchini. Mbali na viongozi hao, Mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongozwa na Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda nao umepata tuzo hiyo kwa kuongoza kwa miradi ya uwekezaji, ambapo takribani miradi 109 imesajiliwa.

MTOTO Juma Megejuwa (12) mkazi wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi