loader
Picha

Tanzania kufaidi Euro milioni 140 za ACP

 JUMLA ya Euro milioni 140 zimetengwa ili kuwanufaisha wakulima wa mazao ya korosho na mahindi katika mpango maalum wa kutoa mikopo, kujenga uwezo katika uzalishaji, masoko, uwekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao hayo kwa wakulima wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific jambo litakalosaidia kupunguza umasikini na njaa katika nchi hizo.

Akizungumza katika mkutano wa 110 wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific uliofunguliwa na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto jijini Nairobi nchini Kenya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania imetoa hoja ya kutaka mazao ya korosho na mahindi kuongezwa katika mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP jambo ambalo limeridhiwa na kuungwa mkono na nchi za Benin na Burkinafaso.

Aliongeza kuwa kukubalika kwa hoja hiyo iliyowezesha mazao hayo kuingizwa katika moja ya mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP, serikali ya Tanzania itajipanga kupitia wizara husika ili kuandaa mapendekezo ya namna ambayo wakulima wa Tanzania watanufaika na programu hiyo sambamba na mazao mengine yakiwemo pamba, miwa na kahawa.

Aidha,Waziri Kabudi alisema kuwa kupitia programu hiyo maalumu ya ACP wakulima wa korosho na mahindi watawekewa mikakati ya kusaidiwa katika uzalishaji, kutafutiwa masoko na mbinu za uwekezaji sanjari na kuongeza mnyororo wa thamani na kusaidiwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kuathiri uzalishaji wa mazao hayo.

Mazao mengine yaliyopo katika mpango wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific kwa muda mrefu sasa licha ya kuwa Tanzania haijatumia fursa hiyo kikamilifu ni pamoja na pamba, kahawa na kakao.

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la Raleigh Tanzania linaendelea na kampeni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi