loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga hali si shwari

YANGA mambo yake yanaonekana kuwa hovyo baada ya nyota wake wa kimataifa kuandika barua za kuomba kuvunja mikataba yao kutokana na kutolipwa mishahara.

Tangu juzi usiku kulikuwa na tetesi kwenye mitandao mbalimbali kwamba nyota wa kimataifa Sadney Urhikob wa Namibia, Lamine Moro wa Ghana na David Molinga wa Congo DR wameandika barua kwa uongozi kutaka kuvunjiwa mikataba yao.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili inazo ni kweli wachezaji hao wameandika barua ya kuvunja mikataba yao na kutwa nzima ya jana viongozi walikuwa na majadiliano kuona namna ya kunusuru hali hiyo.

Gazeti hili lilimtafuta Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela kulizungumzia hilo lakini simu yake ya mkononi haikupokelewa. Lakini msemaji wa Yanga Hassan Bumbuli alisema barua rasmi hazijawafikia na wao wanaziona hizo taarifa mitandaoni.

“Kama mtu anavunja mkataba si anatakiwa alete barua ofisini, sisi barua tunaziona kwenye mitandao kama wanavyoona wengine, lakini kama uongozi tutatoa tamkoa Jumatatu (kesho).”

Alisema kwa sasa wanajiandaa na safari ya Kigoma walikopanga kwenda kucheza mechi za kirafiki kujiweka sawa na ligi na mechi za michuano ya kombe la Shirikisho la Azam, FA zinazotarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 23 na 24 ambapo Yanga itacheza na Iringa United.

“Wanachama wetu wawe watulivu, wasiwe na wasiwasi uongozi uko makini kwa kila kinachotokea watataarifiwa,” alisema Bumbuli.

Suala la wachezaji hao kuomba kusitishiwa mikataba yao huenda likaiathiri Yanga kwani ndio imeanza kukaa sawa kwa siku za karibuni baada ya kumtimua kocha wake Mwinyi Zahera.

Yanga kwa sasa iko chini ya kocha wa muda, mchezaji wake wa zamani Charles Mkwasa ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo kwa pointi 17 na imecheza mechi nane. Kwa sasa ligi imesimama kupisha michuano ya kombe la Chalenji kabla ya kurejea tena Januari mwakani ambapo Yanga itacheza na mtani wake Simba Januari 4.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi