loader
Picha

Kili Stars, Zanzibar Heroes mzigoni leo

TIMU ya soka ya taifa ya Bara Kilimanjaro Stars na ile ya Zanzibar, Zanzibar Heroes leo zinashuka dimbani kwenye viwanja viwili tofauti kucheza michezo ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Chalenji Afrika Mashariki na Kati mjini Kampala.

Michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Zanzibar Heroes dhidi ya Sudan utakaochezwa kuanzia saa 7:30 mchana huku wa pili, Kili Stars dhidi ya Kenya ukitarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.

Utakuwa ni mchezo mgumu kwa kila timu kwasababu kwanza kila mmoja amejipanga kupambana kupata pointi tatu katika mchezo huo wa kwanza.

Kingine ni kwamba, Tanzania na Kenya zinapokutana mechi huwa ngumu kutokana na kujuana na zimeshakutana mara kadhaa katika michuano tofauti iliyopita.

Timu hizo zinakutana pengine kila mmoja ana vikosi tofauti vya vijana pamoja wakongwe wachache kwa hiyo unaweza kuwa na upinzani mkali.

Ziliwahi kukutana michuano miwili ya Cecafa mwaka 2013 na 2017 Kenya ilishinda zote bao 1-0 kila mmoja.

Pia, walikutana mchezo wa kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani zikatoka sare michezo miwili, mmoja walitoka suluhu na mwingine walifungana bao 1-1 kisha zikaingia kwenye penalti na Tanzania kushinda 4-1.

MABINGWA wa kihistoria Yanga kupitia Kampuni ya GSM wamesema wanajipanga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    fredy g
    08/12/2019

    Hao wachezaj wa yanga waliokimbia viongoz waachen wasepe zao maan mmeshindw kuwatoa hayo mapene

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi