loader
Picha

Shangwe uzinduzi uwanja Simba usipime

KLABU ya Simba inafunga mwaka vizuri vizuri baada ya kumiliki uwanja wake kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa miaka 83 iliyopita.

Shangwe la mashabiki na wanachama wa Simba jana ilihamia Bunju kwenye uzinduzi huo, ambapo viwanja viliwili vilitambulishwa kile cha nyasi bandia na nyasi asili. Ilikuwa furaha kwa mamia ya mashabiki na wanachama waliohudhuria kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo huku wakiwa wanacheza, wanaimba na kufurahi pamoja kile walichokiona katika uzinduzi huo uliohudhuriwa pia na wachezaji na viongozi wa Bodi ya klabu hiyo.

Uwepo wa uwanja huo ambao ulinunuliwa na mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali na kuwekwa nyasi bandia na Mwekezaji Mohamed Dewji utasaidia kuokoa Sh 300,000 hadi 500,000 walizokuwa wakitumia kukodi uwanja kwa siku.

Mtendaji wa Simba Senzo Mazingisa alisema “Ni wakati wa kujivunia kwa viongozi wote wa Simba, wachezaji na viongozi wa zamani, mashabiki, wanachama na wachezaji wote kushuhudia tukio la uzinduzi wa uwanja wa Bunju awamu ya kwanza.

Alisema wanachokitizama mbele yao kwa sasa sio mchezo dhidi ya Yanga bali kuhakikisha wanafanya vizuri kwanza katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) dhidi ya Arusha FC utakaochezwa Desemba 23, mwaka huu.

“Simba itacheza mchezo dhidi ya Arusha FC kwenye uwanja wa taifa Desemba 23, mwaka huu wakati ile ya watani ikiwa Januari 4, mwakani hivyo tuelekeze macho na masikio katika mchezo huu wa FA ili kushinda na kuingia 32 bora,”alisema na kuongeza kuwa baada ya mchezo huo ndio wataanza kuizungumzia Yanga.

“Leo (jana) ni siku ya furaha sana kwa wanasimba. Shukrani za pekee ziende kwa mwekezaji wetu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Tunataka unapotaja timu kubwa za Afrika uitaje na Simba Sports Club,” amesema Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda.

Nahodha John Bocco aliwashukuru viongozi wa zamani na wa sasa kwa jitihada za upatikanaji uwanja huo na kuwaomba waendelee kuisaidia klabu hiyo kwa mawazo na kuwaelekeza viongozi wa sasa njia walizopitia wao kama ushauri ili kufikia malengo.

Pia, aliwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi akisema wamekuwa wakiwaunga mkono hata mechi mbalimbali kiasi cha kuwapa morali wachezaji.

MABINGWA wa kihistoria Yanga kupitia Kampuni ya GSM wamesema wanajipanga ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi