loader
Picha

Magufuli asamehe wafungwa 5,533

Rais John Magufuli ametangaza kusamehe wafungwa 5,533 na kuonya kuwa isiwe sababu ya watu kufanya makosa kwa kutegemea kusamehewa.

Ametangaza msamaha huo leo jijini Mwanza wakati anahutubia Taifa kwenye sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

“Sifurahi sana kuongoza nchi ya watu wengi wakililia magerezani. Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu mliopata msamaha huu kujutia makosa yenu mliyoyafanya na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa msamaha huu ambao kimsingi yeye ndie aliyewasamehe”amesema Rais Magufuli.

Amesema wafungwa watakaonufaishwa na msamaha huo ni wafungwa wote waliofungwa kati ya siku moja hadi mwaka mmoja, na wafungwa waliofungwa kwa miaka mingi na tayari wametumikia sehemu kubwa ya vifungo vyao na kubakiza muda usiozidi mwaka mmoja.

“Najua ni idadi kubwa na watu watashangaa lakini nimeguswa kwa moyo wangu ninasamehe wafungwa 5, 533”amesema Rais Magufuli na kubainisha kuwa Mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa wanaosamehewa.

Amesema, kwenye mkoa huo amesamehe wafungwa 713, Dodoma wanasamehewa 385, Morogoro 365, Dar es Salaam 293, Mara 260, Mbeya 259, Kigoma 252, Tanga 245, Geita 230, Rukwa 214, Arusha 208, na Manyara 207.

“Hii ni mara ya kwanza kwa msamaha mkubwa namna hii kutokea na huenda usitokee tena kwa sababu miaka haifanani na kila mwaka una maajabu yake”amesema.

Katika Mkoa wa Tabora Rais Magufuli amesamehe wafungwa 2017, Mwanza 190, Ruvuma 181, Singida 139, Simiyu 136, Lindi 129, Pwani 128, Iringa 110, Songwe 96, Katavi 74, Shinyanga 74, na Njombe wanasamehewa wafungwa 70.

“Na ni matumaini yangu hawa wafungwa 5, 533 wataanza kuondoka kuanzia kesho, na wasiwacheleweshe na kuwawekea mizengwe, na orodha ya majina yao ninayo hapa”amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa bila shaka misamaha waliopata wafungwa na mahabusu itasaidia kupunguza mlundikano wa wafungwa na mahabusu magerezani.

NAIBU Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

2 Comments

 • avatar
  maico paul
  09/12/2019

  hongel rais kwakutoa msamaha kwa wafungwa mngu akujalie maisha malef

 • avatar
  Picha
  09/12/2019

  Ct

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi