loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watanzania washauriwa kuchangamkia mikopo

WANANCHI wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na mabenki pamoja na taasisi za fedha nchini ili kuongeza mitaji yao ya biashara na kipato cha familia zao.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwakilishi kutoka Benki ya NMB nchini, Victor Dilunga wakati alipozungumza kwenye kongamano la mafundi mbalimbali Mkoa wa Dodoma lililofanyika jijini hapa jana.

Dilunga aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na mabenki pamoja na taasisi za kifedha nchini ili kukuza mitaji yao ya biashara, akieleza kuwa wananchi wasiogope kuchukua mikopo inayotolewa kwa sababu ipo kwa ajili yao ili kuwawezesha kiuchumi. Pia aliwataka kuchukua mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo miradi ya biashara na ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuepuka kuingia kwenye madeni na taasisi hizo.

Alisema Benki ya NMB katika kuhakikisha inawasaidia wananchi wa kawaida na kukuza mitaji yao, imeanzisha akaunti iliyopewa jina la Fanikiwa inayofunguliwa kwa kianzio cha Sh 2,000 maalumu kwa biashara ndogo.

Aliongeza kuwa kupitia akaunti hiyo mafundi hao wanaweza kufungua na kufanikiwa kupata mikopo ya kununua vitendea kazi vyao. Aidha, alisema NMB pamoja na kutoa huduma za kifedha inawajengea uwezo wafanyabiashara kwa kuwapa elimu ya kutunza fedha pamoja na elimu kabla ya kutoa mikopo.

Naye fundi cherehani, Getrude Urio alisema kupitia mkopo wa Benki ya NMB amenufaika kwa kununua vitendea kazi pamoja na kujenga nyumba ya kuishi eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Urio aliwataka wenzake kujenga uaminifu katika kukopa na kulipa mikopo kwa sababu ukifanya hivyo utakuwa unaishi kwa amani bila kuwakumbia maofisa wa benki. Meneja wa Mradi wa Fundi Sumaty, Wiseman Ruvanda alisema lengo la kongamano hilo ni kuwaunganisha mafundi mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kazi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi