loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ATCL yasafirisha abiria usiku kucha

KAMPUNI ya Ndege la Tanzania (ATCL) imenogesha maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, zilizofanyika jijini Mwanza, kwa kuhakikisha huduma ya usafi ri inapatikana hadi usiku.

Aidha, ATCL imeongeza safari za ndege kwa mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro na Kagera, ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha abiria wanaokwenda maeneo hayo hawakosi usafiri wakati huu wa msimu wa sikukuu.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema katika sherehe za Uhuru wa Tanzania zilizofanywa jana mjini Mwanza, ATCL ilitoa huduma za usafiri wa abiria kwa kuongeza ndege moja ya ziada.

“Tunaongeza ndege kwenye ruti ya Mwanza, Bukoba na Kilimanjaro kwa sababu msimu huu ni wa abiria wengi hasa wanaokwenda makwao kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka, lakini pia jana kulikuwa na tukio kubwa la maadhimisho ya Uhuru, tuliongeza ndege moja ya ziada kwa ruti ya usiku jana (juzi) kutokana na uhitaji wake na leo (jana) usiku pia tumeongeza ruti nyingine ya kwenda na kurudi Dar,” alisema Kagirwa.

Akifafanua, Kagirwa alisema ruti ya kwenda Mwanza na Bukoba, ina ndege tatu kwa siku na kwamba kwenye sherehe za Uhuru, ruti zote zilijaa na ikaongezwa ndege nyingine ambayo ilisafiri usiku wa juzi.

Alisema kwamba ATCL itaendelea kuangalia mahitaji ya wateja na kuongeza ndege pale inapobidi. Akizungumzia mahitaji ya usafiri huo msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya, Kagirwa alisema kwa ruti ya kwenda Bukoba, abiria ni wengi, akitol mfano kuwa familia moja inaweza kuomba kuwekewa nafasi za watu 15.

“Msimu huu wa sikukuu abiria ni wengi na sisi tumejipanga kuhakikisha wateja wetu hawakosi usafiri, tumeongeza ndege moja kwenye ruti ya kwenda Bukoba kwa ndege inayopita Mwanza kwa sababu familia moja inaomba kuwekewa nafasi hata 15, za kwenda Bukoba, sasa utaona mahitaji ni makubwa,” alisema Kagirwa.

Mbali na kuongeza ndege kwenye ruti ya Bukoba, pia kwenye ruti ya Mwanza inayofanya ruti tatu kwa siku, nayo imeongozwa ndege moja, na ruti ya Entebbe kupitia Kilimanjaro ina ndege tatu zinazoruka asubuhi, jioni na usiku.

Alisema abiria wanaotumia usafiri huo wa ATCL wasiwe na wasiwasi, kwani huduma zimeboreshwa na hakutakuwa na shida ya usafiri, kwa sababu wamejipanga kutoa huduma kwa ruti zote kwa kuzingatia wingi wa wateja.

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi