loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Halmashauri zilizokopa zachambuliwa

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema kwa sasa wako katika hatua ya kuchambua taarifa za halmashauri zilizokopa kwenye benki za biashara.

Hivi karibuni, Jafo alitoa siku saba kwa wakurugenzi wa halmashauri kuwasilisha taarifa za mikopo waliyokopa kwenye taasisi za fedha kugharamia miradi ya maendeleo baada ya kubainika ukiukwaji wa agizo la kupiga marufuku halmashauri kukopa. Pia aliagiza halmashauri zilizochukua mikopo na fedha hazijatumika, kurudisha fedha hizo mara moja na kuonya wakurugenzi watakaobainika kuficha taarifa za mikopo.

Akizungumza na HabariLeo, Jafo alisema: “Ni halmashauri pekee ambazo zilikopa fedha kwenye taasisi za fedha kwa kugharamia miradi ya maendeleo zilizotakiwa kuleta taarifa ya mikopo na halmashauri hizo zimeshafanya hivyo. Kwa sasa kinachofanyika ni kuchambua mikopo hiyo kabla ya kutoa taarifa kamili ya suala hilo.”

Jafo ambaye hakuwa tayari kutaja idadi na halmashauri kwa kutokuwa na taarifa wakati huo, alitoa agizo hilo ikiwa ni baada ya Rais John Magufuli kuzuia wakurugenzi kujihusisha na mikopo ya kwenye benki kwa ajili ya miradi maendeleo, kauli aliyoitoa akiwa Kahama.

Jafo alibainisha kuwa baadhi ya halmashauri zimekiuka agizo lililotolewa na Katibu Mkuu Hazina Desemba 13, mwaka 2016 kwa barua yenye kumbukumbu namba CBC.155/233/101 liliagiza taasisi zote za umma ikiwamo mamlaka za serikali za mitaa kutochukua mikopo kwenye benki za biashara kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo mpaka hapo Katibu Mkuu wa Hazina atakapojiridhisha. Jafo pia aliagiza halmashauri ambazo wamechukua mikopo hiyo na hawajaanza kuitumia, warejeshe fedha hizo katika taasisi walizokopa.

Pia agizo hilo linakwenda pamoja na kupiga marufuku halmashauri kukopa fedha kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali na vitendo hivyo kuanzia sasa havitavumiliwa. Rais Magufuli alipiga marufuku halmashauri kukopa fedha kwenye taasisi za kibenki kwa sababu mikopo hiyo imekuwa mzigo kwenye halmashauri kutokana na deni kulipwa kwa viwango vikubwa Na Anastazia Anyimike vya riba.

KUTOKANA na kazi iliyofanywa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi