loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rwanda kuunganisha umeme na nchi jirani

KITUO cha kuzalisha umeme cha Shango chenye thamani ya Faranga bilioni 13.8 kimezinduliwa katika wilaya ya Gasabo na kitakachokuwa na uwezo wa kuunganisha nishati hiyo na nchi nyingine za jirani, hivyo kukuza soko la nishati ya umeme nchini Rwanda.

Kituo hicho chenye uwezo mkubwa kuliko vyote nchini humo, kina uwezo wa kusafirisha kilovoti 220/110 za umeme na kuwezesha Rwanda kupokea na kuuza nishati hiyo katika nchi za Uganda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ujenzi wa kituo hicho utachukua miezi saba kwa kuwa na njia mbili za kusafirisha umeme kuunganishwa na Uganda kupitia milima ya Mirama na Mashariki Kaskazini mwa DRC kupitia kituo cha Rubavu.

Njia mbili nyingine zitaunganisha mtandao wa Rwanda na Magharibi mwa Tanzania na Burundi kupitia mradi wa umeme wa maji katika maporomoko ya Rusumo. Waziri wa Miundombinu, Claver Gatete, alisema mradi huo ni muhimu katika ukanda huo, kukuza biashara mipakani pamoja na upatikanaji wa vyanzo nafuu vya nishati.

Alisema kituo hicho ni cha kimataifa kitakachounganisha nchi jirani kikiwa na volti 220 na kuifanya Rwanda kuwa na vituo 28 vya kuzalisha umeme, huku ikilenga kuwa na vituo 44 ifikapo 2024.

foto
Mwandishi: GASABO

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi