loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bodaboda kuwekewa mita malipo ya nauli

PIKIPIKI (Bodaboda) 36,000 zinatarajiwa kuwekewa vifaa maalumu vya kielektroniki (mita) zitakazotumika kusoma umbali na mteja kulipia fedha ili kuepuka matumizi ya fedha taslimu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wizara ya Miundombinu kuingia makubaliano ya miaka miwili na kampuni mbili za teknolojia kutoka Afrika Kusini za Pascal Technology Ltd Rwanda na Altron.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, kampuni hizo zitafanya uwekezaji wa Dola za Marekani milioni 18 kwa ajili ya mita hizo ili kufikia lengo la sekta ya usafiri kuachana na malipo ya fedha taslimu.

Mhandisi Mkuu wa Usalama na Leseni Wizara ya Miundombinu, Francois Zirikana, juzi alisema uwekezaji huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kuboresha sekta ya usafiri wa pikipiki.

Aprili, mwaka huu, Baraza la Mawaziri lilipitisha mkakati wa kitaifa wa usafiri wa pikipiki ili kusaidia serikali kufikia lengo la kufikia uchumi wa kutotumia fedha taslimu mwaka 2024. Wafanyabiashara ya bodaboda wamepewa hadi Julai, mwakani kuhakikisha wameweka mfumo huo wa malipo bila kutumia fedha taslimu.

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi