loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania Bara, Kenya mambo safi Cecafa U-17

TIMU ya Tanzania Bara ya wasichana waliochini ya Umri wa miaka 17 na ile ya Kenya zimeanza vema mashindano ya Baraza la Vyama vya soka vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) baada ya kushinda mechi zao jana ziliochezwa Viwanja vya FUFA Technical Centre, Njeru, Jinja, Kampala.

Tanzania Bara ndio ilifungua pazi la mashindano hayo mapya ya wasichana kwa kucheza na Eritrea na kuifunga mabao 5-0 mchezo uliochezwa saa 5:00 asubuhi.

Katika mchezo huo mabao mawili ya Tanzania Bara yalifungwa na Aisha Masaka dakika ya 21 na 41 na Joyce Meshack 29, 54 na 62 na kuandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga ‘hat trick’ kwenye mashindano hayo.

Kenya wao waliifunga Djibouti kwa mabao 14-0 yaliyofungwa na Anna Arusi katika dakika za 17, 44 na 68, Fasila Adhiambo katika dakika za 20, 41, 52 na 68, Lavin Anyango dakika ya 38, Viola Khalai aliyefunga katika dakika za 25, 40, 43, 50 na 53 na Dorine Achieng dakika ya 81.

Akizungumza baada ya mchezo huo kocha Bakari Shime, alisema aliwashukuru wachezaji kwa kucheza vema hadi kupata ushindi na kusisitiza lengo lao ni kurudi na ubingwa.

“Kwanza niwapongeze wachezaji kwa ushindi lakini wanatakiwa kujua lengo letu ni kurudi na ubingwa hivyo kama ni mapambano ndio yameanza hakuna kurudi nyuma,” amesema Shime maarufu kama mchawi mweusi.

Pia Shime amesema wamekwenda Uganda kucheza vizuri, kushindana na kuchukua ubingwa na wamejiandaa vema, hivyo hawana kisingizio.

Mashindano hayo ambayo yanachezwa kwa mtindo wa ligi yatamalizika Desemba 17 na yanatarajiwa kuendelea kesho ambapo Tanzania Bara itacheza na Burundi, Kenya itaivaa Eritrea na Uganda itacheza na Djibouti.

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amesema ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi