loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Makongoro Mahanga naye yamkuta Chadema

NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira wa zamani, Dk Makongoro Mahanga, naye ameangukia pua katika uchaguzi mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) unaoendelea. Dk Mahanga ameshindwa katika uchaguzi wa Baraza la Wazee, uliofanyika Dar es Salaam jana.

Mahanga ambaye alizaliwa Aprili 3, 1955, alikuwa mbunge wa Jimbo la Segerea Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM kwa miaka kumi hadi mwaka 2015, alipojiengua na kukimbilia Chadema.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye aliyekimbilia Chadema mwaka huo 2015, naye aling’oka baada ya kufanyiwa ‘figisu’ kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

Dk Mahanga alikuwa mmoja wa watu walioeleza kiini cha Sumaye kuangushwa katika Chadema. Akizungumzia uchaguzi huo Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene alisema Chadema kimemchagua Roderick Lutembeka kuwa Katibu wa Baraza la Wazee aliyepata kura 113 na kumshinda mshindani wake, Dk Mahanga aliyepata kura 26.

Alisema nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara, imeendelea kushikiliwa na Suzan Lyimo kwa awamu nyingine aliyepata kura 135, sawa na ushindi wa asilimia 100. Suzan ni mbunge wa Viti Maalum.

Alisema kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Wazee aliyeshinda ni Hashim Juma Issa, aliyepata kura 112 na mshindani wake Hugho Kimaryo alipata kura 15. Kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, mshindi ni Idrisa Mkila aliyepata kura 74 dhidi ya Mwanamrisho Taratibu Abama aliyepata kura 64. Naibu Katibu Mkuu Bara mshindi ni Hellen Kayanza aliyepata kura 78 dhidi ya mshindani wake Andrew Kimbombo aliyepata kura 60.

Aidha Naibu Katibu Mkuu Zanzibar mshindi ni Haji Kali Haji aliyepata kura 116 dhidi ya Hamad Mbarouk aliyepata kura 22. Mweka hazina wa Baraza la Wazee ni Erasto Gwota. Aidha, leo mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), atabainika na nafasi hiyo inawaniwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, peke yake.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wagombea wake ni wanne ambao ni Hawa Subira Mwaifunga, Aisha Yusuf Luja, Mary Nyagabona na Marceline Stanslaus. Wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar wagombea ni watatu, ambao ni Maryam Salum Msabaha, Sharifa Suleiman Suleiman na Zeud Mvano Abdulahi.

Nafasi ya Katibu Mkuu inawaniwa na Grace Tendega. Alisema wagombea wa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara wako sita na kwa Naibu Karibu Mkuu Zanzibar wagombea ni wawili ni Asya Mwadini Mohammed na Bahati Chumu Haji.

Kuhusu utaratibu za uchaguzi, alisema Desemba 19 mwaka huu Baraza Kuu litachagua Katibu Mkuu na Naibu Katibu wa chama hicho. Kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi kwa Kanda ya Pwani, alisema ni kweli taratibu zitafanyika baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa viongozi ngazi ya taifa.

JESHI la Polisi limejipanga kusimamia utekelezaji wa sheria ili kuzuia ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi