loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

U-17 Tanzania Bara, Burundi zatoka sare

TIMU ya Tanzania Bara ya wasichana walio chini ya Umri wa miaka 17 imetoka sare ya kufungana mabao 3-3 na timu ya Burundi katika mchezo wa Michuano ya Kombe la Chalenji, jijini Kampala, Uganda jana.

Mchezo huo wa kusisimua kwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati uliochezwa kwenye Viwanja vya FUFA Technical Centre, Njeru, Jinja jijini Kampala. Katika mchezo huo mabao ya Tanzania Bara yalifungwa na Joyce Meshack dakika ya 17, Aisha Masaka dakika ya 50 na Christer John na yale ya Burundi yalifungwa na Bora Ineza, Lydia Karenzo na Neema Nzohabona.

Kwa matokeo hayo, Tanzania Bara ina pointi nne katika michezo miwili, sawa na Kenya ambayo imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Eritrea huku Burundi ikiwa na pointi moja.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha wa Tanzania Bara, Bakari Shime alisema anamshukuru Mungu kwa kumaliza mchezo kwa sare na kuwapongeza wapinzani wao kwa kutumia vema nafasi walizopata.

“Namshukuru Mungu tumecheza mchezo vizuri na tumemaliza kwa sare lakini niwapongeze Burundi kwani walikuwa nyuma kwa matokeo 3-1 lakini walipambana na kurudisha mabao hayo na kumaliza kwa sare 3-3,” alisema na kuongoza: ”Lazima nikakae na wachezaji wangu ili kujipanga na mchezo dhidi ya Kenya kwani kutoka sare leo haimaniishi tumetoka kwenye mashindano”.

Katika orodha ya kuwania ufungaji bora, mchezaji wa Kenya, Viola Khalai anaongoza akiwa na mabao matano, akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Fasila Adhiambo mwenye mabao manne sawa na wachezaji wa Tanzania Bara, Joyce Meshack na Aisha Masaka.

Wenye mabao matatu ni Anna Arusi wa Kenya akiwa na mchezaji wa Uganda, Juliet Nalukenge Doreen Achieng na Sylvia Makhungu wa Kenya wana bao moja sawa na Samalie Nakacwa wa Uganda na Christer John wa Tanzania Bara na Bora Ineza, Lydia Karenzo na Neema Nzohabona wote wa Burundi.

Mashindano hayo ambayo yanachezwa kwa mtindo wa ligi, yatamalizika Desemba 17 na yanatarajiwa kuendelea kesho ambapo Tanzania Bara itacheza na Kenya, Eritrea itaivaa Uganda na Djibouti itacheza na Uganda.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Nigeria, Junior Lokosa ametua ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi